• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 12:11 PM
KWPL: Kisumu All Starlets kupimana nguvu na WADADIA Women

KWPL: Kisumu All Starlets kupimana nguvu na WADADIA Women

NA AREGE RUTH

MECHI tano za Ligi Kuu ya Wanawake nchini (KWPL), zimepangwa kupigwa katika nyuga tofauti tofauti nchini.

Kesho Jumamosi, Kisumu All Starlets watawaalika WADADIA Women ugani Moi mjini Kisumu saa sita mchana. 

Kisumu watakuwa wanatafuta alama tatu muhimu ilikujiondoa kwenye hatari ya kushushwa daraja. Kwenye mechi za awali za ligi, Kisumu walipigwa 2-1 na Ulinzi Starlets ugani Ulinzi Sports Complex nao WADADIA wakatoka sare ya 1-1 dhidi ya Bunyore Starlets nyumbani.

Mechi ya kukata na shoka mnamo Jumapili ni kati ya mabingwa watetezi Thika Queens na wanajeshi wa Ulinzi Starlets ugani Thika kaunti ya Kiambu.

Timu hizi zilikutana mara ya mwisho katika uwanja huo tarehe nane mwezi Mei mwaka jana na mechi hiyo ikakamilika 0-0.

Baada ya aliyekuwa kocha wa Thika Joseph Oyoo kujiuzulu mwaka jana, kocha mpya Richard Kanyi alichukua mikoba yake. Kanyi  aliongoza Thika kunyakuwa ubingwa wa ligi mwaka 2016 na baadae aliondoka kwenye klabu hiyo tarehe mbili mwezi wa pili msimu wa 2020/21 na kurejea tena mwaka huu.

Alianza kazi vibaya kwa kupoteza nyumbani siku ya Jumatano waliponyeshea 2-1 na Bunyore Starlets. Ulinzi nao watatafuta ushindi ambao utawaweka kileleni mwa jedwali.

Kocha wa Ulinzi Joseph Mwanzia anasema, “Hii itakuwa ni mechi ngumu kwa kuwa kila mtu anapigania taji. Hizi ni timu mbili nzuri sasa kwenye ligi, tumejiandaa vilivyo kupambana na wapinzani wetu.”

Kwa upande mwingine, Gaspo Women watapumzika wikendi hii. Walipangwa kucheza dhidi ya Trans Nzoia Falcons lakini mechi ikahairishwa  kufuatia matukio katika kambi ya Falcons wikendi iliyopita. Falcons wataanza tena majukumu ya ligi Jumatano, Januari 25, 2023.

Debi kati ya Bunyore Starlets na Vihiga Queens itapigwa ugani Mumboha, Luanda kaunti ya Vihiga.

Vihiga ambao wameonyesha nia ya kutwaa ubingwa msimu huu, hawajapoteza mechi zao nne za awali. Kwa upande wa Bunyore walianza msimu vizuri na wanashikilia nafasi ya nne bora kwenye jedwali.

Kocha Mkuu wa Bunyore Zakaria Zilasi anasema amepata pigo kuwa baada ya mchezaji wake Susan Malda kupata jeraha.

“Ni pigo kubwa kwa timu yetu na kawa sasa natafuta njia ya kujaza pengo hilo. Malda atakuwa nje kwa muda baada ya kuumia kwenye mechi yetu dhidi ya Thika. Wachezaji pia wamekuwa na uchovu mwingi baada ya safari ndefu, wamerejea mazoezini jana na tuko tayari kucheza kesho,” alisema Zilasi

Nakuru City Queens watafunga kazi dhidi ya Kayole Starlet FC katika uwanja wa Maonyesho ya Kilimo (ASK) mjini Nakuru.

  • Tags

You can share this post!

Fulham waendeleza masaibu ya kocha Graham Potter kambini...

DOUGLAS MUTUA: Korona ingali tishio duniani, tunafaa...

T L