• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 5:50 AM
Liverpool wamaliza kampeni za Kundi A kwenye UEFA katika nafasi ya pili licha ya kukomoa Napoli ugani Anfield

Liverpool wamaliza kampeni za Kundi A kwenye UEFA katika nafasi ya pili licha ya kukomoa Napoli ugani Anfield

Na MASHIRIKA

LIVERPOOL walikomesha rekodi nzuri ya Napoli katika Klabu Bingwa Ulaya (UEFA) kwa kuwapepeta 2-0 katika mchuano wa mwisho wa Kundi A uliowakutanisha ugani Anfield mnamo Jumanne usiku.

Chini ya kocha Jurgen Klopp, Liverpool walikuwa na kiu ya kujinyanyua baada ya Leeds United kuwatandika 1-0 katika Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) mnamo Oktoba 29, 2022.

Bao kutoka kwa Mohamed Salah na Darwin Nunez yaliwezesha miamba hao kufuta rekodi ya Napoli ya kutoshindwa katika mechi 21 za mashindano yote.

Liverpool walishuka dimbani wakiwa na ulazima wa kubebesha Napoli gunia la angalau mabao matatu ugani Anfield ili kukamilisha kampeni ya Kundi A kileleni na kuepuka kibarua cha kukutana na ama Real Madrid, Bayern Munich au Paris Saint-Germain (PSG) katika hatua ya 16-bora.

Hata hivyo, huo uliishia kuwa mtihani mgumu kwa masogora wa Klopp waliodhibitiwa vilivyo na Napoli hadi dakika ya 85 ambapo Salah alifunga bao kabla ya Nunez kuongeza la pili sekunde chache kabla ya kipenga cha kuashiria mwisho wa mchezo kupulizwa. Sasa wana alama 15 sawa na Napoli. Ajax ni wa tatu katika Kundi A kwa alama sita huku Rangers wakivuta mkia bila pointi yoyote.

Mchuano dhidi ya Liverpool ulikuwa wa kwanza kwa Napoli wanaoselelea kileleni mwa jedwali la Ligi Kuu ya Italia (Serie A) kupoteza katika UEFA muhula huu.

Liverpool walitinga hatua ya 16-bora ya UEFA kwa msimu wa sita mfululizo chini ya Klopp wiki moja iliyopita baada ya kutandika Ajax 3-0 mjini Amsterdam, Uholanzi. Hata hivyo, miamba hao wamekuwa wakisuasua ligini muhula huu na walipigwa na Leeds United 2-1 mnamo Oktoba 29, 2022 ugani Anfield.

Matokeo hayo yalikomesha rekodi ya kutoshindwa kwa Liverpool katika EPL uwanjani Anfield kwa miaka mitano na nusu. Ilikuwa mechi ya kwanza kwa beki Virgil van Dijk kupoteza katika ligi ugani Anfield tangu ajiunge na Liverpool mnamo 2018.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Mto Ewaso Nyiro waendelea kukauka athari hasi za mabadiliko...

IPOA: Polisi 18 wamesukumwa jela kwa kukiuka haki za...

T L