• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 2:31 PM
Madereva chipukizi wa Kenya waelekea Estonia kushangilia McRae Kimathi

Madereva chipukizi wa Kenya waelekea Estonia kushangilia McRae Kimathi

Na GEOFFREY ANENE

MADEREVA Jeremiah Wahome, Maxine Wahome na Hamza Anwar wameratibiwa kuondoka nchini leo Julai 11 usiku kuelekea Estonia.

Watatu hao watashuhudia duru ya saba ya Mbio za Magari Duniani (WRC) ya Rally Estonia itakyofanyika Julai 14-17.

Watakuwa mashabiki huku bingwa wa Afrika wa kitengo cha chipukizi 2021 McRae Kimathi akipaisha gari lake la Ford Fiesta R3 akishirikiana na Mkenya mwenzake Mwangi Kioni.

Kampuni ya Safaricom na Kenya Airways imelipia madereva hao wanne kutoka Kenya gharama yote kuwa Estonia ikiwemo nauli ya ndege na malazi.

“Tunasubiri kwa hamu kubwa kushuhudia Rally Estonia. Tunafurahia kuwa tunaenda kupata uhondo wa mbio za magari nchini humo,” alisema Jeremiah mnamo Jumatatu.

Kimathi atakabiliana na dereva anayeongoza kitengo cha chipukizi duniani (JWRC) Jon Armstrong kutoka Uingereza pamoja na Robert Virves (Estonia), Sami Pajari na Lauri Joona kutoka Finland, na William Creighton (Ireland).

Chipukizi hao wote wataendesha magari ya Ford Fiesta Rally3 kutoka kampuni M-Sport Poland. Watapewa magurudumu kutoka kwa Pirelli. Creighton, Joona, Pajari, Kimathi na mshiriki mpya Roope Korhonen pia wanaweza kujishindia pointi za kitengo cha WRC3 Open.

  • Tags

You can share this post!

Man-United wampa Ronaldo makataa ya kurejea kambini au la,...

Ombi Wajackoyah azimwe kuwania urais kwa sababu ni hatari...

T L