• Nairobi
  • Last Updated May 16th, 2024 8:50 PM
Makinda wang’arisha Arsenal Carabao Cup

Makinda wang’arisha Arsenal Carabao Cup

LONDON, UINGEREZA

Na MASHIRIKA

USHINDI mnono wa Arsenal wa 5-1 dhidi ya Sunderland mnamo Jumanne usiku katika robo-fainali ya kombe la Carabao, umedhihirisha umuhimu wa kuekeza katika soka la vijana.

Makinda wote waliopewa nafasi ugani Emirates walionyesha kiwango cha juu na kumuacha kocha Mikel Arterta na kibarua cha kuchagua nani atafaa zaidi kwa mechi ipi siku za usoni.Eddie Nketiah, 22, ndiye alifungua ukurasa wa magoli dakika ya 17.

Dakika 10 baadaye winga Nicholas Pepe, 26, alifanya mabao kuwa mawili.Sunderland wakarejesha goli moja kupitia kwa Nathan Broadhead dakika ya 31.Lakini wanabunduki wa Arsenal waliendeleza ukatili wao Nketiah alipopiga goli la tatu na la nne la timu – na kukamilisha hattrick yake – kabla kinda Charlie Patino, 18, kuhitimisha ubabe wa Gunners kwa bao la dakika ya 90.

Patino alikuwa ameingia uwanjani dakika ya 80 na haikumchukua muda kudhihirishia kocha Arteta uwezo wake, hii ikiwa mara yake ya kwanza kuchezea kikosi cha kwanza cha Arsenal.Baada ya kutinga bao hilo Patino alisema ni ushindi ambao ataukumbuka milele maishani mwake.Kocha Arteta alikuwa na sifa kedekede kumhusu, akitaja bao hilo kama “ndoto spesheli.”Alieleza:

Kucheza mechi yako ya kwanza hapa (Emirates), na kufunga mbele ya mashabiki wetu, ni jambo spesheli mno!”Hata hivyo, aliomba mashabiki kuwa watulivu ili kumpa muda wa kuzidi kuiva.“Sasa lazima tuendelee kumuivisha kwa upole,” akasema Mhispania huyo akitoa ishara ya chungu motoni.

Kumhusu staa mwingine usiku huo, Nketiah, Arteta alisema: “Ni kweli mkataba wake unaelekea ukingoni, lakini uamuzi wa hali yake ya baadaye ni wake mwenyewe.“Lengo lake ni kusakata kandanda na daima anataka kucheza. Jukumu ni lake kuamua, lakini ni mchezaji ambaye tungependa aendelee kuwa kikosini.

Jinsi anavyocheza hata mazoezini, ni mchezaji anayestahili muda wa kutosha uwanjani.”Ushindi wa Arsena umewawezesha kutinga hatua ya nusu-fainali ya michuano hiyo ya Carabao Cup kwa mara ya nane kwa jumla; ya kwanza tangu msimu wa 2007-08.

Gunners watatumai makinda wataendelea kusisimua na kuonyesha weledi wao ili kufika fainali, na kushinda kombe hilo kwa mara ya tatu katika historia yao. Arsenal waliongoza kwa 2-0 mapema kutokana na mabao ya Nketiah na Nicolas Pepe.

Historia imethibitisha kwamba vipaji vingi vya wachezaji waliochezea Arsenal ilipokuwa ikivuma miaka ya hapo nyuma vilitokana na matokeo ya uwekezaji mkubwa wa kituo chao cha kuvumbua na kukuza chipukizi.Lakini wengi wa wachezaji wa kikosi kikuu cha sasa wametokea katika sehemu tofauti wakisajiliwa kwa haraka bila mbinu zao kuchunguzwa kwa makini kama ilivyokuwa nyakata hizo.

Nyakati za Arsene Wenger kituo cha Arsenal kilikuwa na akademia bora ambayo ilizalisha wachezaji wengi walioiletea timu hiyo sifa katika mashindano mbali mbali barani Ulaya.Ufanisi wao ulitokana na mafunzo mazuri waliopata ya kucheza soka lenye mbinu za kupiga pasi katika mazingara magumu na mepesi.

You can share this post!

Afrika yajadili haja ya mfumo bora wa afya

Wanawe 19 wamletea faraja ingawa alikosa ushauri bora...

T L