• Nairobi
  • Last Updated May 16th, 2024 8:50 PM
Martial apata jeraha akichezea Ufaransa dhidi ya Kazakhstan

Martial apata jeraha akichezea Ufaransa dhidi ya Kazakhstan

Na MASHIRIKA

FOWADI Anthony Martial wa Manchester United alipata jeraha wakati akichezea timu yake ya taifa ya Ufaransa dhidi ya Kazakhstan katika mchuano wa kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia za 2022.

Martial alichangia bao la kwanza ambalo Ufaransa walifungiwa na mshambuliaji wa Barcelona, Ousmane Dembele dhidi ya Kazakhstan wanaoshikilia nafasi ya 122 duniani.

Bao la pili la Ufaransa lilitokana na tukio la Sergiy Maliy kujifunga baada ya kuzidiwa na presha kutoka kwa Martial katika dakika ya 44.

Baada ya kuumia, nafasi ya Martial ilitwaliwa na mfumaji chipukizi wa Paris Saint-Germain (PSG), Kylian Mbappe ambaye alishuhudia penalti yake ikipanguliwa na kipa wa Kazakhstan mwishoni mwa kipindi cha pili.

Baada ya kulazimishiwa na Ukraine sare ya 1-1 mnamo Machi 24, Ufaransa ambao ni washikilizi wa Kombe la Dunia, sasa wanajivunia alama nne kutokana na mechi mbili zilizopita za Kundi D.

Chini ya kocha Didier Deschamps, Ufaransa wanatarajiwa kurejea uwanjani mnamo Machi 31 kuvaana na Bosnia-Herzegovina ugenini.

Kiungo wa Man-United, Paul Pogba, anatarajiwa kuwa sehemu ya kikosi cha Ufaransa katika mechi hiyo. Sogora huyo wa zamani wa Juventus alichezeshwa na Ufaransa kwa dakika 60 dhidi ya Kazakhstan kabla ya kuondolewa uwanjani na nafasi yake kutwaliwa na Adrien Rabiot.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Olmo awabeba Uhispania dhidi ya Georgia

Uganda kukosa kunogesha fainali za AFCON kwa mara ya kwanza...