• Nairobi
  • Last Updated April 28th, 2024 3:31 PM
Mwanariadha Alfred Kipketer apigwa marufuku kwa kukiuka kanuni za kudhibiti matumizi ya pufya

Mwanariadha Alfred Kipketer apigwa marufuku kwa kukiuka kanuni za kudhibiti matumizi ya pufya

Na CHRIS ADUNGO

MWANARIADHA Alfred Kipketer amepigwa marufuku ya miaka miwili kwa hatia ya kukiuka kanuni za kudhibiti matumizi ya pufya.

Kitengo cha Maadili (AIU) katika Shirikisho la Riadha Duniani (WA) kilimwadhibu Kipketer ambaye aliibuka bingwa wa dunia katika mbio za mita 800 kwa chipukizi wasiozidi umri wa miaka 20 mnamo 2014 kwa kosa la kutojiwasilisha mara nne kwa vipimo vya afya.

Awali, Kipketer alikuwa tu amezuiwa kwa muda kutoshiriki mashindano yoyote katika ulingo wa riadha. Hata hivyo, AIU ilimpata na hatia na kumpokeza adhabu hiyo kali inayoanza sasa kutekelezwa mnamo Novemba 26, 2019 hadi Novemba 25, 2021.

Kwa kuwa Kipketer alikiri kwamba alikosa kujiwasilisha kwa vipimo vya afya mnamo Februari 3, 2020, AIU imempokeza adhabu na maamuzi hayo yanaanza kutekelezwa Novemba 26.

Ina maana kwamba Kipketer kwa sasa anapokonywa medali, mataji na tuzo zote alizowahi kujizolea kuanzia Novemba 26, 2019.

Kipketer anakuwa mwanariadha wa kwanza wa haiba kubwa nchini Kenya kupigwa marufuku na AIU mwaka huu wa 2021.

Mnamo 2019, AIU ilimpiga marufuku Elijah Manangoi aliyeibuka bingwa wa dunia katika mbio za mita 1,500 mnamo 2017 kwa kosa hilo hilo la kukiuka kanuni zinazodhibiti matumizi ya pufya.

Mshikilizi wa zamani wa rekodi ya dunia katika marathon Wilson Kipsang na Daniel Wanjiru aliyetawazwa bingwa wa London Marathon mnamo 2017 pia walipigwa marufuku ya miaka minne kila mmoja mnamo 2020 kwa hatia ya kutumia dawa za kusisimua misuli.

  • Tags

You can share this post!

Serikali yatoa hela za ujenzi wa shule zilizoathiriwa na...

Elijah Manangoi apigwa marufuku ya miaka miwili kwa hatia...