• Nairobi
  • Last Updated May 9th, 2024 6:40 PM
Naomi Osaka aingia raundi ya tatu ya tenisi ya mchezaji mmoja kila upande kirahisi

Naomi Osaka aingia raundi ya tatu ya tenisi ya mchezaji mmoja kila upande kirahisi

Na MASHIRIKA

NAOMI Osaka wa Japan alitinga raundi ya tatu ya Olimpiki kwenye tenisi ya mchezaji mmoja kila upande baada ya kumpiku Viktorija Golubic wa Uswisi.

Osaka ambaye anapigiwa upatu wa kutwaa dhahabu baada ya kudenguliwa kwa Ashleigh Barty kwenye raundi ya kwanza, alimpokeza Viktorija kichapo cha 6-3, 6-2.

Atakutana sasa na Marketa Vondrousova au Mihaela Buzarnescu katika kivumbi cha kuwania tiketi ya robo-fainali.

Garbine Muguruza na Anastasia Pavlyuchenkova pia walisajili ushindi katika raundi ya tatu. Kabla ya kujitosa ulingoni kwa Olimpiki, Osaka alikuwa amepumzika kwa wiki nane ili kujiweka sawa kiakili.

“Hii ni fursa spesheli kwangu kutwaa dhahabu ya Olimpiki ambayo nimekuwa nikisubiri kwa takriban miaka minane sasa,” akasema Osaka.

Bingwa mara mbili wa Grand Slam, Muguruza wa Uhispania, alimbwaga Wang Qiang wa China 6-3, 6-0 chini ya kipindi cha dakika 61.

Mwanafainali wa French Open, Pavlyuchenkova wa Urusi alihitaji muda wa dakika 54 pekee kumcharaza Anna-Lena wa Ujerumani 6-1, 6-1.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

You can share this post!

Rhonex Kipruto kuwa kizibo cha nyota Geoffrey Kamworor mbio...

Polisi wadaiwa kurusha kilipuzi katika baa