• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 5:50 AM
Odera ang’atuka Kenya Simbas baada ya kukosa tiketi ya Kombe la Dunia

Odera ang’atuka Kenya Simbas baada ya kukosa tiketi ya Kombe la Dunia

Na GEOFFREY ANENE

KOCHA Paul Odera ameagana na timu ya taifa ya raga ya wachezaji 15 kila upande almaarufu Kenya Simbas baada ya miaka mitatu usukani.

Odera, ambaye kandarasi yake ilifaa kukatika mwezi huu baada ya mashindano ya mwisho ya kufuzu kushiriki Kombe la Dunia 2023 yaliyofanyika Novemba 22-18 mjini Dubai, alijiuzulu mara tu Simbas ilipopigwa 22-18 na Hong Kong katika mechi ya mwisho Jumamosi.

Simbas ilipata pointi zake dhidi ya Hong Kong kupitia kwa John Okoth na Jacob Ojee (mguso mmoja kila mmoja) na Geoffrey Ominde (penalti mbili na mkwaju mmoja). Iliongoza mara mbili katika mechi hiyo kabla ya kusalimu amri kupitia alama za Luke Van Der Smit, Sean Taylor na Jak Lam (mguso mmoja kila mmoja) na Gregor McNeish (penalti moja na mikwaju miwili).

Ureno ilitwaa tiketi ya kushiriki Kombe la Dunia 2023 nchini Ufaransa baada ya kutoka 16-16 katika fainali dhidi ya Amerika. Wote wawili walimaliza kwa pointi 12, lakini Ureno ilikuwa na tofauti nzuri ya ubora wa magoli. Hong Kong ilikamilisha kwa alama nne.

Odera alishuhudia vijana wake wakikosa tiketi ya moja kwa moja kupitia Kombe la Afrika baada ya kupoteza 36-0 dhidi ya Namibia katika fainali mwezi Julai nchini Ufaransa. Kisha, walianza vibaya mashindano ya mwisho mjini Dubai walipolimwa 68-14 na Amerika kabla ya kuaibishwa 85-0 na Ureno. Mwenyekiti wa Shirikisho la Raga Kenya (KRU) Geoffrey Oduor Gangla amesema Jumamosi kuwa shirikisho hilo litatoa tangazo kuhusu mwelekeo mpya wa Simbas juma lijalo.

You can share this post!

Qatar yapigwa na Ecuador na kuwa timu ya kwanza kuwahi...

BAHARI YA MAPENZI: Je, unakosa furaha katika mahusiano?

T L