• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 12:48 PM
Okutoyi atafaidi usaidizi wa Serikali kwenye US Open

Okutoyi atafaidi usaidizi wa Serikali kwenye US Open

Na GEOFFREY ANENE

WAZIRI wa Michezo Amina Mohamed ameahidi kuwa mwanatenisi Angella Okutoyi atapata usaidizi kutoka kwa serikali kwenye kampeni zake za shindano la haiba la US Open mwezi Septemba.

Alikuwa akizungumza katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta mnamo Jumatatu usiku baada ya kulaki Okutoyi aliyeandikisha historia kwa kuwa Mkenya wa kwanza kufika fainali ya Grand Slam na pia kushinda wakati wa Wimbledon wikendi iliyopita.

“Hongera Okutoyi kwa taji hili. Tunajivunia kazi yako. Umepatia taifa motisha. Rais Uhuru Kenyatta anafahamu nimekuja hapa na amelezea furaha yake. Wizara itakusaidia utakapokuwa unaelekea US Open. Tutakutana naye pamoja na sekta ya kibinafsi ili kufanya mipango ya baadaye,” alisema waziri.

Akishirikiana na Mholanzi Rose Marie Nijkamp, walitawala fainali ya Wimbledon kitengo cha wachezaji wawili kila upande cha chipukizi kwa kulemea raia wa Canada Kayla Cross na Victoria Mboko 3-6, 6-4, 11-9 jijini London.

Okutoyi alifurahia kuandikisha historia hiyo kwenye uwanja wa nyasi wa klabu ya All England na anatumai kukamilisha mwaka kwa kishindo.

You can share this post!

BORESHA AFYA: Vyakula vya kuongeza nguvu za kiume

Waliokuwa maafisa wa serikali ya Kidero wahukumiwa miaka 30...

T L