• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 6:50 AM
Omanyala avunja rekodi 100m Austria

Omanyala avunja rekodi 100m Austria

Na GEOFFREY ANENE

MKENYA Ferdinand Omurwa Omanyala alisherehekea rekodi mpya ya kitaifa ya mbio za mita 100 baada ya kutimka kwa sekunde 9.86 akishinda fainali kwenye mashindano ya JOSKO Lauf-Meeting nchini Austria, Jumamosi.

Omanyala alikuwa ametimka 9.96 katika nusu-fainali. Mkimbiaji huyo mwenye umri wa miaka 25 alikosa pembamba kufika fainali kwenye Olimpiki 2020 nchini Japan mnamo Agosti 1 baada ya kukamilisha umbali huo kwa sekunde 10.00.

Kupitia mtandao wake wa Twitter, alieleza kufurahishwa na muda wake mpya akisema, “Hatimaye, nimefanikiwa kumaliza mbio za mita 100 chini ya sekunde 10. Nimetimka 9.96!!!! Ilikuwa tu lazima rekodi ipatikane nchini Austria. Fainali za mbio hizi zinafuatana hivi karibuni. Asante Mungu.”

Hiyo ilikuwa mara ya tatu mwaka 2021 Omanyala alivunja rekodi ya kitaifa kabla ya kuimarisha kwa mara ya nne akitwaa taji nchini Austria kwa 9.86.

Alianza mwaka kwa kutimka 10.01 kwenye mashindano ya MoC Grand Prix mwezi Machi nchini Nigeria akivunja ile ya 10.14 ambayo Mark Otieno aliweka mwaka 2017.

Ferdinand Omurwa Omanyala asherehekea kuvunja rekodi ya kitaifa katika mbio za mita 100 nchini Austria, Agosti 14, 2021. Picha/Hisani

Kisha, Omanyala alitimka 10.00 katika nusu-fainali ya Olimpiki jijini Tokyo alikibwaga shujaa wake Yohan Blake kutoka Jamaica.

Rekodi mpya ya 9.96 itamnyanyua kutoka nafasi ya 23-bora mwaka huu duniani hadi nambari 17 juu ya Mwamerika Justin Gatlin anayekamata nafasi ya 20 kwa sekunde 9.98.

Usain Bolt (Jamaica) na Akani Simbine (Afrika Kusini) wanashikilia rekodi ya dunia ya 9.58 na 9.84, mtawalia. Hapo jana, Omanyala alifuatwa kwa karibu na Mwingereza Jamal Rhoden-Stevens (sekunde 10.34) na Tomas Nemejc katika nusu-fainali ya kundi la nne.

Katika fainali ya Kundi A, Omanyala alikamilisha tena mbele ya Rhoden-Stevens (10.32) aliyefuatiwa na Adam Raska kutoka Jamhuri ya Czech (10.83), Steve Camilleri kutoka Malta (10.96), mwenyeji Enakhe Edegbe (10.96) na Mejrumani David Kantzog (10.99).

Baada ya Austria, Omanyala amesema anaelekea jijini Helsinki nchini Finland.

You can share this post!

Edwin Ng’ang’a Thuo: Nahodha anayeinua...

Gor Mahia yatoka sare, huku Bandari ikipepeta Mathare