• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 12:48 PM
Raga: Odera akiri makosa yaliponza Kenya Simbas dhidi ya Namibia

Raga: Odera akiri makosa yaliponza Kenya Simbas dhidi ya Namibia

Na GEOFFREY ANENE

KOCHA Paul Odera amekiri kuwa vijana wake wa Kenya Simbas walifanya makosa mengi yaliyochangia wapoteze 36-0 dhidi ya Namibia mnamo Julai 10 usiku kwenye fainali ya Kombe la Afrika ambayo mshindi alitinga Kombe la Dunia 2023.

Katika mahojiano na Odera, ameeleza Taifa Spoti, “Tulicheza vizuri dakika 20 za kwanza. Mbinu zetu za ulinzi zilikuwa nzuri na tulikuwa tukicheza katika sehemu zinazofaa uwanjani. Hata hivyo, tulifanya makosa wakati muhimu baada ya hapo. Tulichengwa, tulikosa kuondosha mipira ya kupiga vyema nje na pia tulikuwa na makosa ya kukamata mpira. Tuliadhibiwa na timu nzuri kwa makosa hayo yote.”

Namibia, ambayo ilifunga alama zake kupitia kwa nahodha Wian Conradie (miguso mitatu na penalti tatu), Cliven Loubser (penalti na mkwaju) na nahodha Johan Deysel (mguso), itamenyana na wenyeji Ufaransa, washindi mara tatu New Zealand pamoja na Italia na Uruguay katika mechi za Kundi A mwaka ujao.

Simbas ina fursa ya mwisho ya kufuzu mwezi Novemba kwenye mashindano ya muondoano dhidi ya Ureno na mshindi kati ya Hong Kong na Tonga na pia atakayeshinda kati ya Amerika na Chile. Timu itakayotawala mashindano hayo ya mataifa manne pia itajikatia tiketi ya Kombe la Dunia. Itaingia Kundi C lililo na Wales, Australia, Fiji na Georgia.

Katika msimamo wa mwisho wa Kombe la Afrika, Namibia ilihifadhi taji ikifuatiwa na Kenya. Algeria ilimaliza nambari tatu baada ya kuduwaza Zimbabwe 20-12, Uganda ikazima Ivory Coast 18-17 katika mechi ya kuorodhesha nambari tano na sita nayo Senegal ikapepeta Burkina Faso 44-30 katika mechi ya kuamua nafasi mbili za mwisho.

  • Tags

You can share this post!

LISHE: Faida za mafenesi kwa binadamu

IEBC yasema imeweka mikakati ya kuzuia changamoto katika...

T L