• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 8:55 PM
Real Madrid wapiga Getafe na kukaribia Atletico kileleni mwa jedwali la La Liga

Real Madrid wapiga Getafe na kukaribia Atletico kileleni mwa jedwali la La Liga

Na MASHIRIKA

REAL Madrid walipaa hadi nafasi ya pili kwenye msimamo wa jedwali la Ligi Kuu ya Uhispania (La Liga) na kupunguza pengo la alama kati yao na viongozi Atletico Madrid baada ya kuwachapa Getafe 2-0 uwanjani Alfredo di Stefano.

Chini ya kocha Zinedine Zidane, Real ambao ni mabingwa watetezi wa La Liga, walianza mchuano huo bila ya kujivunia huduma za wachezaji kadhaa wa kikosi cha kwanza kutokana na majeraha na marufuku.

Hata hivyo, walitamalaki mchezo na kumiliki asilimia kubwa ya mpira katika vipindi vyote viwili.

Karim Benzema alifungua karamu ya mabao katika dakika ya 60 kabla ya beki Ferland Mendy kuongeza la pili dakika sita baadaye.

Real kwa sasa wanajivunia alama 46, tano nyuma ya Atletico ambao wana mechi mbili zaidi ya kusakata ili kufikia idadi ya michuano 22 ambayo imepigwa na watani wao hao kutoka jijini Madrid.

Kutokuwepo kwa wanasoka wazoefu Eden Hazard, Sergio Ramos, Federico Valverde, Toni Kroos na Alvaro Odriozola kulimweka kocha Zidane katika ulazima wa kukumbatia mfumo wa 3-4-3 ambao ni mpya zaidi kwa kikosi cha Real.

Zidane alitumia mchuano huo kuwapa chipukizi Marvin Park, 20, na Victor Chust, 20, nafasi ya kudhihirisha ukubwa wa uwezo wao uwanjani.

Kushindwa kwa Getafe kuliwasaza katika nafasi ya 13 jedwalini kwa alama 24 sawa na Valencia na Cadiz.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

You can share this post!

COVID-19: Mechi za Europa League kati ya Real Sociedad na...

Juventus yadengua Inter Milan na kuingia fainali ya Coppa...