• Nairobi
  • Last Updated May 16th, 2024 8:50 PM
Sancho aweka rekodi ya uchangiaji mabao katika soka ya Bundesliga

Sancho aweka rekodi ya uchangiaji mabao katika soka ya Bundesliga

Na MASHIRIKA

JADON Sancho, 20, alifunga bao na kuchangia bao lake la 50 katika mechi za Ligi Kuu ya Ujerumani (Bundesliga) mnamo Jumamosi wakati ambapo waajiri wake Borussia Dortmund waliwapepeta limbukeni Arminia Bielefeld.

Sancho ambaye ni raia wa Uingereza alikuwa akicheza mechi yake ya 99 katika La Liga. Alichangia bao la kwanza la waajiri lililofungwa na Mahmoud Dahoud katika dakika ya 48 kabla ya yeye mwenyewe kucheka na nyavu za Arminia katika dakika ya 58 kupitia penalti.

Penalti hiyo ilikuwa zao la nahodha Marco Reus kuchezewa visivyo na Amos Pieper.

Reinier Jesus anayechezea Dortmund kwa mkopo kutoka Real Madrid aliwafunga Arminia bao la tatu lilichangiwa na fowadi matata raia wa Norway, Erling Braut Haaland.

Dortmund kwa sasa wanashikilia nafasi ya tano kwenye msimamo wa jedwali la Bundesliga kwa alama 39, tatu nyuma ya nambari nne Eintracht Frankfurt.

MATOKEO YA BUNDESLIGA (Februari 27):

Bayern 5-1 FC Koln

Stuttgart 5-1 Schalke

Wolfsburg 2-0 Hertha Berlin

Leipzig 3-2 M’gladbach

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

You can share this post!

Mbappe afunga mawili na kusaidia PSG kurefusha mkia wa...

Juventus wakabwa koo na Verona katika Serie A