• Nairobi
  • Last Updated May 4th, 2024 1:14 PM
Spurs wamvizia kocha Paulo Fonseca kuwa mrithi wa Jose Mourinho

Spurs wamvizia kocha Paulo Fonseca kuwa mrithi wa Jose Mourinho

Na MASHIRIKA

TOTTENHAM Hotspur sasa wanamvizia kocha zamani wa AS Roma, Paulo Fonseca, kwa nia ya kumpokeza mikoba yao ya ukufunzi.

Spurs wanaoshiriki Ligi Kuu ya Uingereza (EPL), wanapania kutafuta mrithi wa mkufunzi Jose Mourinho ambaye tayari amefanywa kizibo cha Fonseca kambini mwa Roma tangu apigwe kalamu jijini London, Uingereza mnamo Aprili 19, 2021.

Ingawa Fonseca aliridhisha pakubwa kambini mwa Roma, kocha huyo raia wa Ureno alitimuliwa mwishoni mwa msimu wa 2020-21 baada ya waajiri wake kuambulia nafasi ya saba kwenye msimamo wa jedwali la Ligi Kuu ya Italia (Serie A).

Roma pia walibanduliwa na Manchester United ya Uingereza kwenye nusu-fainali za Europa League.

Fonseca alijaza nafasi ya kocha Claudio Ranieri kambini mwa Roma baada ya kudhibiti mikoba ya Shakhtar Donetsk ya Ukraine kwa kipindi cha miaka mitatu. Amewahi pia kuwatia makali wanasoka wa Porto na Braga nchini Ureno.

Chini ya ukufunzi wake, aliongoza Shakhtar kushinda jumla ya mataji mawili mnamo 2016 kabla ya kurudia ufanisi huo mnamo 2019. Alinyanyua pia taji la Portuguese Cup akidhibiti mikoba ya Braga mnamo 2016 kisha akatwaa Portuguese Super Cup akiwa kocha wa Porto mnamo 2013.

Spurs tayari wamemwajiri Fabio Paratici kuwa mkurugenzi wao wa soka. Kinara huyo alitokea Juventus ya Italia ambako alihudumu kwa kipindi cha miaka 11.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Mishi Mboko amshauri Shahbal awe mtiifu kwa ODM

Wenyeji watumai kuzima mzozo na wasimamizi wa ‘shamba...