• Nairobi
  • Last Updated April 27th, 2024 11:15 AM
Udinese wadidimiza matumaini ya AC Milan kutwaa taji la Serie A msimu huu

Udinese wadidimiza matumaini ya AC Milan kutwaa taji la Serie A msimu huu

Na MASHIRIKA

FURSA ya AC Milan kutia kibindoni ufalme wa Ligi Kuu ya Italia (Serie A) kwa mara ya kwanza msimu huu tangu 2010-11 ilitiwa doa na sare ya 1-1 waliyolazimishiwa Jumatano usiku katika mechi iliyowakutanisha na Udinese ugani San Siro.

Penalti ya nyota Franck Kessie katika dakika ya 97 iliwasaidia AC Milan ya kocha Stefano Pioli kusawazisha mambo na kuondoka uwanjani wakiwa na alama moja muhimu.

Awali, dalili zote zilikuwa zikiashiria kwamba Udinese wangetoka uwanjani wakijivuni alama zote tatu kapuni mwao baada ya Rodrigo Becao kuwaweka wageni uongozini katika dakika ya 68.

AC Milan kwa sasa wanashikilia nafasi ya pili jedwalini kwa alama 53, tatu nyuma ya viongozi Inter Milan walio na mchuano mmoja zaidi wa kutandaza ili kufikia idadi ya mechi ambazo zimepigwa na washindani wao wakuu wakiwemo AC Milan, Atalanta na AS Roma.

Mabingwa watetezi Juventus wanashikilia nafasi ya tatu kwa alama 49 sawa na Atalanta wanaofunga mduara wa nne-bora.

Ushindi kwa Inter katika mechi ya Machi 4, 2021 dhidi ya Parma, utawezesha masogora hao wa kocha Antonio Conte kufungua mwanya wa alama sita kileleni mwa jedwali la Serie A.

Zikisalia mechi 14 kabla ya kampeni za Serie A muhula huu kumataika, Juventus wanaowinda taji lao la 10 mfululizo wanatenganishwa na Inter kwa alama saba zaidi.

Inter hawajawahi kutwaa ufalme wa Serie A tangu 2009-10. Watapania kuweka hai matumaini ya kutawazwa mabingwa wa wa muhula huu watakapovaana na Juventus mnamo Mei 16, 2021 jijini Turin.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Man U watamaushwa na sare ya Palace

Kivumbi kuendelea miongoni mwa klabu tatu za kwanza Ligue 1