• Nairobi
  • Last Updated May 9th, 2024 6:40 PM
Kivumbi kuendelea miongoni mwa klabu tatu za kwanza Ligue 1

Kivumbi kuendelea miongoni mwa klabu tatu za kwanza Ligue 1

Na MASHIRIKA

VIKOSI vitatu vya kwanza kwenye msimamo wa jedwali la Ligi Kuu ya Ufaransa (Ligue 1) vilisajili ushindi katika mechi za Machi 3, 2021 na kuendeleza vita vikali vya kuwania ubingwa wa taji la msimu huu.

Lille, Paris Saint-Germain (PSG) na Olympique Lyon wote walishinda mechi zao za Jumatano dhidi ya Olympique Marseille, Bordeaux na Rennes mtawalia.

Mechi kati ya Lille na Marseille ilielekea kukamilika kwa sare tasa kabla ya fowadi matata raia wa Canada, Jonathan David kufunga mabao mawili ya haraka mwishoni mwa kipindi cha pili.

Lille kwa sasa wanajivunia alama 62 kileleni mwa jedwali huku pengo la pointi mbili likitamalaki kati yao na nambari mbili PSG waliopepeta Bordeaux 1-0 kupitia bao la Pablo Sarabia.

Lyon wanakamata nafasi ya tatu kwa alama 59 baada ya kucharaza Rennes 1-0. Goli la pekee na la ushindi katika mechi hiyo lilipachikwa wavuni na Houssem Aouar.

Kila mojawapo ya timu zinazoshikilia nafasi tatu za kwanza kwenye msimamo wa jedwali la Serie A, imesalia na mechi 10 pekee za kupiga kabla ya kampeni za msimu huu kutamatika rasmi.

PSG wanaotiwa makali na kocha wa zamani wa Tottenham Hotspur, Mauricio Pochettino, wametawazwa mabingwa wa Ligue 1 kwa misimu mitatu iliyopita mfululizo. Miamba hao watakuwa wageni wa Lyon mnamo Machi 21 kabla ya kualika Lille mnamo Aprili 4, 2021. Kwa upande wao, Lyon wamepangiwa kuwa wenyeji wa Lille mnamo Aprili 25, 2021.

MATOKEO YA LIGUE 1 (Machi 3):

Bordeaux 0-1 PSG

Brest 3-1 Dijon

Lyon 1-0 Rennes

Metz 0-1 Angers

Nice 2-1 Nimes

Saint-Etienne 2-3 Lens

Lille 2-0 Marseille

Montpellier 1-1 Lorient

Nantes 1-2 Reims

Strasbourg 1-0 Monaco

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGOA

  • Tags

You can share this post!

Udinese wadidimiza matumaini ya AC Milan kutwaa taji la...

Barcelona wanyonga Sevilla na kutinga fainali ya Copa del...