• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 9:50 AM
Waendesha pikipiki wa Kenya watupia jicho mashindano ya Afrika

Waendesha pikipiki wa Kenya watupia jicho mashindano ya Afrika

Na GEOFFREY ANENE

BAADA ya kukamata nafasi ya pili katika mbio za pikipiki za Central Africa Motocross Challenge (CAC) jijini Kampala nchini Uganda, waendesha pikipiki kutoka Kenya sasa wanaelekeleza talanta zao kwa mashindano ya Afrika (MXOAN).

Mashindano ya Afrika yataandaliwa mjini Cape Town, Afrika Kusini mwezi Agosti 11-13.

Yatakuwa mashindano ya pili ya kimataifa kwa Wakenya mwaka 2023 baada ya CAC mjini Busiika, Uganda ambayo walitumia kupima uwezo wao kabla ya kampeni ya Cape Town.

Mkurugenzi wa Beyond Sports katika Shirikisho la Mbio za Pikipiki barani Afrika (FIM) anayesimamia tume za wanawake katika uendeshaji wa pikipiki, mazingira, matibabu, burudani na utalii, Julie Wahome, amesema baada ya kushiriki mashindano ya CAC nchini Uganda wakati wa likizo ya Pasaka, Kenya itaandaa raundi ya pili ya CAC mwezi Desemba.

“Hiyo itakuwa baada ya mashindano ya Afrika mwezi Agosti mjini Cape Town,” akasema.

Akizungumza kwa niaba ya Shirikisho la michezo ya mbio za magari na pikipiki nchini Afrika Kusini (MSA), Neville Townsend alisema wanasubiri kwa hamu kubwa washiriki wa kitaifa, bara na kimataifa.

Wakati wa mashindano ya CAC katika eneo la Busiika, wenyeji walinyakua taji la jumla kwa alama 1,627 dhidi ya Kenya (495).

Mkenya Berry Notea alimaliza kitengo cha MX50 katika nafasi ya pili, Wahome Mutahi na Lewis Ogonyi wakaridhika nambari mbili na tatu mtawalia (MX85), Mungai Magithuku akawa nambari tatu (MX1) nao Alex Kandie na Masalule Kituyi wakakamata nambari mbili na tatu mtawalia (MX2).

  • Tags

You can share this post!

Mtindo bora wa maisha yasiyo na shinikizo hatari

‘Matilda Sakwa arejeshwe awe Mkurugenzi Mkuu wa...

T L