• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 2:31 PM
Wananyuki yazidi kuwika baada ya kuwanyuka wapinzani wao wa jadi Omax

Wananyuki yazidi kuwika baada ya kuwanyuka wapinzani wao wa jadi Omax

NA ABDULRAHMAN SHERIFF

WANANYUKI waliendelea kufanya vizuri kwenye Ligi ya FKF ya Taifa Daraja la Pili Kanda ya Kaskazini walipopata ushindi wao wanne mfululizo kwa kuwachapa wapinzani wao wa jadi Omax FC kwa mabao 2-0 kwenye mechi iliyochezwa uwanja wa shule ya msingi ya Tudor.

Wananyuki walianza kwa kufanya mashambulizi na haikuwa ajabu kunako dakika ya 28, walipopata bao la kuongoza lilofungwa na Heshima Said kutokana na sokomoko lilokuwako langoni mwa Omax.

Omax ilipungukiwa na mchezaji mmoja dakika moja kabla ya mapumziko wakati Omar Mohammed Mwambindo alipotolewa nje kwa kupoewa kadi nyekundu na refarii kutoka Kilifi  Vincent Nyika baada kumuonyesha kadi ya pili ya njano.

Saadh Abdalla alihakikishia timu yake inapata ushindi alipotinga nyavu kukiwa kumebakia dakika tano mchezo huo kumalizika. Omax ilijitahidi kutaka kusawazisha lakini mabeki wa Wananyuki hawakutoa upenyo.

Kutokana na ushindi huo, Wananyuki iko kwenye nafasi ya pili kati ya timu 19 zinazoshiriki kwenye ligi hiyo ikiwa na pointi 13 sawa na walizonazo viongozi Progressive FC ya Malindi lakini wana mabao machche.

Wananyuki ya Mombasa imecheza mechi tano, imeshinda mechi nne na kutoka sare mchezo mmoja. Wananyuki inakutana na  Progressive katika mchezo unaotarajia kuwa wa kuvutia kati ya timu hizo mbili zinazoongoza ligi hiyo ambao utachezwa uwanja wa MTTI Bomani.

  • Tags

You can share this post!

Newcastle United waridhishwa na sare tasa dhidi ya West...

Osoro aachiliwa kwa dhamana