• Nairobi
  • Last Updated May 4th, 2024 9:55 AM
Wasichana wa Kenya waendelea kung’aria wapinzani tenisi ya U14 na U16 Kigali

Wasichana wa Kenya waendelea kung’aria wapinzani tenisi ya U14 na U16 Kigali

Na GEOFFREY ANENE

WASICHANA kutoka Kenya waliendelea kufanya vyema katika mashindano ya tenisi ya Afrika Mashariki ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 14 na miaka 16 katika vitengo vya wasichana jijini Kigali, Rwanda, Alhamisi.

Faith Urasa alimlemea Ndikumasabo Chiara 6-1, 6-0 naye Reha Kipsang akalima Akeza Zaituni 6-4, 6-0 katika makabiliano ya mchezaji mmoja kwa mmoja wasiozidi umri wa miaka 16.

Urasa alishirikiana na Hadassa Msine kupiga Zaituni na Umuvyeyi Kinsey 6-0, 6-1 katika mechi ya wachezaji wawili wa kitengo hicho. Ulikuwa ushindi wa pili wa timu hiyo ya wasichana ya Kenya iliyopepeta Comoros 3-0 katika siku ya kwanza Mei 4.

Katika michuano mingine ya kitengo hicho mnamo Alhamisi, Uganda ilibwaga Comoros 3-0, nayo Rwanda ikazamisha Tanzania 2-1.

Katika mechi za wavulana za umri umri huo, Wakenya Gilbert Wechuli na Liberty Kibue hawakuwa na lao walipopoteza 6-4, 6-4 na 6-2, 6-1 dhidi ya Abdul Shakur na Allan Gatoto kutoka Burundi mtawalia.

Kibue na Wechuli walilemewa 6-1, 6-3 dhidi Junior Hakizumwami/C. Ishimwe katika kitengo cha wachezaji wawili kwa wawili. Hiyo ni mechi ya pili ya wavulana ya Kenya kupoteza baada ya kuchapwa na Rwanda 3-0 Jumatano. Rwanda ilizaba Tanzania 3-0 katika mchuano mwingine wa wavulana wa umri huo Alhamisi.

Katika umri wa miaka 14 na chini, Wakenya Ayush Bhandari na Baraka Ominde walizidia maarifa Waganda Jonah Ssetongo na Abdul Latif 6-0, 6-2, mtawalia. Ominde na Brian Nyakundi walizima Latif na Tony Blair 6-1, 6-1 katika mechi ya wachezaji wawili kwa wawili.

Kenya pia iling’ara katika kitengo cha wasichana baada ya Seline Ahoya kunyamazisha Uganda 6-1, 6-1, naye Melissa Mwakha akaliza Abigail Nabasinga 6-0, 6-0. Mwakha na Stacy Yego walishirikiana kubwaga Nabasinga/Afwoyoroth 6-1, 6-1.

Rwanda ilipoteza 2-1 dhidi ya Tanzania katika kitengo cha wasichana na pia wavulana kwa mechi 2-1.

  • Tags

You can share this post!

Rais Kenyatta awasilisha bungeni majina ya watu 22...

DOMO: Sista-du Avril, usanii ni kujitolea

T L