• Nairobi
  • Last Updated May 4th, 2024 10:15 PM
BBI yasababisha mpasuko miongoni mwa madiwani wa Mlima Kenya

BBI yasababisha mpasuko miongoni mwa madiwani wa Mlima Kenya

MWANGI MUIRURI na CHARLES WASONGA

MGAWANYIKO sasa umeibuka miongoni mwa madiwani kutoka eneo la Mlima Kenya kuhusiana na kampeni za mpango wa maridhiano (BBI) ambazo zimesababisha tofauti kati ya Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto.

Mswada wa marekebisho ya Katiba kupitia ripoti ya BBI sasa sharti ulipitishwa na angalau mabunge 24 ya kaunti kabla ya kuwasilishwa katika Bunge la Kitaifa na Seneti.

Hiini baada ya Tume ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) kuidhinisha sahihi 1.4 milioni za wapiga kura wanaounga mkono mchakato huo.

Baadaye mswada huo tawasilishwa kwa wananchi kwa kura ya maamuzi mwishoni mwa Juni mwaka huu.

Huku Dkt Ruto akiwa ameanzisha mchakato wa kushawishi madiwani wa kaunti mbalimbali wakatae mswada huo, wale wa mrengo wa rais Kenyatta wameanzisha mpango wa kukabiliana na pingamizi hizo; unaongozwa na mwenyekiti mwa Muungano wa Madiwani wa Mlima Kenya, Charles Mwangi.

Bw Mwangi ambaye ni diwani wa wadi ya Ichagaki kaunti ya Murang’a ambaye amepuuzilia mbali mkutano wa Jumamosi wa madiwani wanaoegemea mrengo wa Dkt Ruto. Ametaja madiwani hao kama “kundi la walaghai ambao wanataka kuuza Mlima Kenya bila kuzingatia masilahi ya kisiasa ya eneo hilo siku zijazo.”

Mkutano wa madiwani hao ulifanyika katika mkahawa wa Thika Green chini ya udhamini wa Mbunge wa Gatundu Kusini Moses Kuria.

Chini ya mwavuli wa vuguvugu la Mt Kenya Progressive MCAs Forum, madiwani hao wameahidi kupambana na wenzao wa mrengo wa Rais Kenyatta unaoongozwa na Bw Mwangi.

Diwani huyo amepuuzilia mbali juhudi za Dkt Ruto za kushawishi mabunge ya kaunti katika eneo la Mlima Kenya yakatae BBI kama, “hadaa ya kisiasa inayoongozwa na tamaa ya kisiasa na haja ya kupanda mbegu ya uhasama na kuwachochea wakazi dhidi ya rais na serikali.”

Hata hivyo, mrengo wa Dkt Ruto, ukiongozwa na Bw Kuria ulisema kuwa mkutano wao mjini Thika ulikuwa moja kati ya mikutano mingi inayoandaliwa kuimarisha ushawishi wa vuguvugu la hasla kote nchini.

Ishara

Hii inaashiria mwanzo wa makabiliano kati ya makundi haya mawili katika uwanja wa kisiasa kuelekea kura ya maamuzi kuhusu BBI.

“Tunafahamu hatua ambazo BBI imepitia kabla ya kugeuzwa kuwa mswada. Mswada wa kuwezesha kufanyika kwa kura ya maamuzi ungali bungeni na utapitishwa Julai mwaka. Baada ya mswada huo kuwasilishwa katika mabunge ya kaunti utawasilishwa bunge la kitaifa.Kwa hivyo, tumekuja pamoja kunalena kuhakikisha kuwa wananchi wengi wanahusishwa katika mpango huu wote sio watu wachache,” akasema Bw Kuria.

Mbunge huyo alisema madiwani wandani wa Dkt Ruto ambao wamekuwa wakifanya mikutano maeneo mbalimbali nchini wanalenga kusambaza jumbe kuhusu sera za vuguvugu la hasla hadi katika ngazi za wadi.

Kwa upande wake mbunge wa Mathira Rigathi Gachagua alisema mrengo wa Naibu Rais hauna nia ya kumpiga vita Rais na wandani wake, akisema “lengo letu ni kuboresha mustakabali wa kisiasa na kiuchumi wa watu wetu.”

  • Tags

You can share this post!

AKILIMALI: Mboga ainati za kiasili ndizo tegemeo la riziki

Leicester City na Everton nguvu sawa ligini