• Nairobi
  • Last Updated May 4th, 2024 9:55 AM
IEBC yachapisha majina ya wabunge na maseneta maalum

IEBC yachapisha majina ya wabunge na maseneta maalum

Na CHARLES WASONGA

TUME Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) imechapisha kwenye gazeti rasmi la serikali majina ya wabunge na maseneta maalum, saa chache kabla ya kikao cha kwanza kufanyika Alhamisi, Septemba 8, 2022.

Kulingana na ilani hiyo iliyotiwa saini na mwenyeketi wa tume hiyo Wafula Chebukati, vyama vikuu vimegawa nafasi 12 katika Bunge la Kitaifa na 16 za wanawake katika seneti.

Vyama pia vimegawa maseneta maalum wanaowakilisha vijana na walemavu katika seneti.

Mwenyekiti  wa ODM John Mbadi na aliyekuwa Mbunge Mwakilishi wa Murang’a Sabina Chege ni miongoni mwa wabunge maalum sita watakaowakilisha mrengo wa Azimio la Umoja One Kenya katika Bunge la Kitaifa.

Wengine ambao watahudumu kama wabunge  maalum katika mrengo wa Azimio ni Irene Mayaka (ODM), Umulkher Mohamed (ODM) na Seleka Harun (United Democratic Movement-UDM).

Nafasi ya Wiper iliachwa wazi kutokana na kesi iliyowasilishwa korti kupinga chaguo cha chama hicho.

Wale ambao watawakilisha mrengo wa Jubilee kama wabunge maalum ni babake mwanamuzi tajika wa injili Emmy Kosgei, Jackson Kosgei, (UDA), Teresa Wanjiru Mwangi (UDA), Dorothy Ikiara (UDA), Joseph Wainaina Iraya (UDA) na Joseph Hamisa Denar (ANC).

Katika bunge la Seneti mwenyekiti wa Bodi ya Kitaifa ya Uchaguzi wa ODM (NEB) Catherine Mumma  ni miongoni wa watu 11 walioteuliwa na mrengo wa Azimio kuwa maseneta maalum.

Wengine ni; Mwenyekiti wa kundi la wanawake wa ODM Betty Syengo, Beatrice Akinyi Oyomo (ODM), Hamida Ali Kibwana (ODM) na Betty Batuli Montet (ODM).

Wengine ni aliyekuwa Seneta wa Uasin Gishu Margaret Kamar (Jubilee), Mariam Shakila Omar (UDM) na Shakila Abdallah (Wiper).

Katibu Mkuu wa United Democratic Alliance (UDA) Veronica Maina anaongoza orodha ya maseneta maalum watakaowakilisha mrengo wa Kenya Kwanza. Wengine ni; aliyekuwa Mbunge Mwakilishi wa Narok Roselinda Soipan Tuya (UDA),  aliyekuwa Mbunge Mwakilishi wa Bomet Joyce Korir, aliyekuwa mwaniaji wa kiti cha Mbunge Mwakilishi wa Kike Nairobi Karen Nyamu, aliyekuwa Mbunge wa Kajiado Mashariki Peris Tobiko, Gloria Magoma Orwoba na Maureen Tabitha Mutinda.

Watakaohudumu kama maseneta wanaowakilisha vijana ni; Bi Hezena Lemaletian (ODM) na Bw Raphael Chimera Mwinzagu (UDA).

Na wale ambao watawakilisha watu wanaoishi na ulemavu ni: Bi Crystal Kagehi Asige (ODM) na George Mungai Mbugua (UDA).

  • Tags

You can share this post!

Mwanahabari BBC asimulia jinsi watoto wanavyoibwa kutoka...

IEBC: Mpigakura aomba Mahakama Kuu itimue Chebukati, Marjan

T L