• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 8:55 PM
ODM wadai Matiang’i anatumia polisi kuwahangaisha Kisii

ODM wadai Matiang’i anatumia polisi kuwahangaisha Kisii

Na WYCLIFFE NYABERI

Waziri wa Usalama wa Ndani, Dkt Fred Matiang’i na Gavana wa Kisii, Bw James Ongwae, wametofautiana vikali huku kampeni za uchaguzi mdogo wa eneobunge la Bonchari zikizidi kuchacha.Uchaguzi huo mdogo umeratibiwa kufanyika Jumanne, wiki ijayo.

Vyama vya Jubilee na ODM vilipoamua kuwateua wawaniaji katika uchaguzi mdogo wa Bonchari kinyume na jinsi vimekuwa vikifanya katika chaguzi ndogo za hivi karibuni kufuatia handisheki, wadadisi walisema kuwa hatua hiyo ingeleta joto la kisiasa na tayari hilo limeanza kutimia.

Alhamisi, maafisa wa polisi wapatao 50 walivamia nyumbani kwa Bw Ongwae katika eneo la Maili Mbili baada ya kupokea ripoti kuwa gavana huyo alikuwa na nia ya kuandaa mkutano wa kupanga jinsi ya kumvumisha mwaniaji wa chama cha ODM mhandisi Pavel Oimeke.

Seneta wa Kisii Prof Sam Ongeri, Mwakilishi wa Kike Kisii, Bi Janet Onge’era na mwenzake kutoka Migori, Bi Pamela Odhiambo walifukuzwa kutoka nyumbani kwa Gavana Ongwae.

Licha ya Gavana Ongwae kuwaeleza kuwa hawakuwa na nia yoyote ya kupanga siasa ila alikuwa amewaalika marafiki zake kwa ajili ya chakula cha jioni, polisi hao walishikilia kuwa hawangeondoka ikiwa Prof Ongeri, Bi Ongera na Bi Odhiambo hawangesalimu amri.

Wakiongozwa na katibu mkuu wa chama cha ODM, Bw Edwin Sifuna, viongozi hao walidokeza kuwa serikali imekuwa ikiwahangaisha na kudai kwamba kunayo njama ya kuiba kura za Bonchari ili kumfaa mwaniaji wa chama cha Jubilee, Bw Zebedeo Opore.Malalamishi kama hayo yametolewa pia na wafuasi wa chama kinachohusishwa na Naibu Rais, Dkt William Ruto cha UDA.

Lakini Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) bado haijatoa ripoti yoyote kuhusu tuhuma hizo hata baada ya kuandikiwa barua ya malalamishi na chama cha ODM siku chache zilizopita.

Gavana Ongwae alidokeza kuwa hatua ya maafisa wa polisi kuvamia boma lake ni mbaya inayomdhalalisha na kutisha kuwa huenda akatathmini upya uhusiano wake na Dkt Matiang’i ikiwa wanachama wa ODM watazidi kuhujumiwa. Gavana Ongwae amekuwa kwenye mstari wa mbele kuongoza juhudi za kumtawaza Dkt Matiang’i kama msemaji wa jamii ya Gusii.

“Mimi ni gavana niliyechaguliwa na wakazi wengi wa Kisii na watu fulani wanapotumwa kwangu wakisema wamepewa amri kutoka juu, ninahuzunishwa. Ikiwa haya yataendelea, basi sitakomea hapo,” akasema Bw Ongwae.

Kumekuwa na madai kwamba serikali imekuwa ikiwahangaisha wawaniaji wengine kwenye kampeni za uchaguzi wa Bonchari ilhali ikimlinda na kumpigia debe mwaniaji kupitia chama tawala cha Jubilee Bw Zebedeo Opore.

Baadhi ya wawaniaji wamelalama kuwa serikali imekuwa ikitumia nguvu zake na maafisa wa polisi ili kuwatia woga wanaopingana na Bw Opore kwa kutawanya kampeni zao.

Seneta Ongeri naye alitoa kauli sawia na gavana na kusema kila mwaniaji wa Bonchari anafaa kupewa wakati rahisi kufanya kampeni zake kwa amani.

Mwakilishi wa Kike Bi Ong’era alimtahadharisha waziri Matiang’i asitumie polisi vibaya na kuwataka polisi kukoma kutawanya mikutano yao kwa kutupa gesi za kutoa machozi. Kampeni hizo zinafika kikomo leo usiku (Jumamosi).

Bw Sifuna alidokeza kuwa chama chao kilikuwa radhi kumenyana na kile cha Jubilee kwenye misingi aliyoitaja ni ya kirafiki. Baada ya kukashifu vumanizi kwa gavana, Bw Sifuna aliongeza kuwa hawatakubali kamwe jaribio lolote la wizi wa kura.

“Hatutakaa kitako tuone serikali ikihujumu uamuzi wa watu kama ilivyofanya katika eneobunge la Matungu. Tumesukumwa ukutani na hatuwezi kuendelea kusukumwa tena,” akasema Bw Sifuna.

Aidha Bw Sifuna aliongeza kuwa hawatakubali serikali iwatumie maafisa wake ili wamtafutie kura mtu fulani.Haya yanajiri baada ya kusemekana kuwa njama nyingine iliyokuwa ikitumiwa na serikali kuhakikisha inakitwaa kiti cha Bonchari ni kuwatumia machifu na Nyumba Kumi kuwarai wapiga kura wamchague mwaniaji wake.

Viongozi hao waliiomba IEBC ijitokeze na kutoa taarifa ni kwa nini baadhi ya wawaniaji wamekuwa wakihangaishwa.Aidha viongozi hao wameitaka tume hiyo kuchukua uongozi imara wa kuulinda na kufanikisha uchaguzi hu

You can share this post!

Kuzimwa kwa Reggae pigo kwa Ruto licha ya kusherehekea

Serikali yapandisha bei ya mafuta baada ya majaji kurarua...