• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 7:50 AM
Sonko ajiengua kutoka kwa Jubilee

Sonko ajiengua kutoka kwa Jubilee

NA CHARLES WASONGA

ALIYEKUWA gavana wa Nairobi Mike Sonko amejiuzulu kama mwanachama wa chama tawala cha Jubilee.

Katika barua aliyomwandikia Katibu Mkuu wa chama cha hicho Jeremiah Kioni, Bw Sonko alisema amechukua hatua hiyo ili kupata nafasi ya kuwa mwanachama wa chama cha kisiasa ambacho anataka.

“Nimechukua hatua hii ya kujiuzulu kama mwanachama wa Jubilee ili niweze kujiunga na chama kingine kitakachoniwezesha kuendeleza ndoto zangu za kisiasa. Ninashukuru chama cha Jubilee kwa kunidhamini kuwania ugavana wa Nairobi,” akasema katika barua hiyo.

Hata hivyo, Bw Sonko hakufichua ni chama kipi atajiunga nacho ikizingatiwa kuwa juzi alitangaza kuwa atawania ugavana wa Nairobi kwa mara nyingine.

Gavana huyo aling’atuliwa afisini mnamo Desemba 20, 2021 kwa tuhumu za kushiriki ufisadi na kutumia vibaya mamlaka ya afisi yake.

Mapema wiki hii serikali ya Amerika ilimzima Bw Sonko na familia yake kuzuru taifa hilo kwa tuhuma zizo hizo za ufisadi.

Mwanasiasa huyo anakabiliwa na kesi kadhaa za ufisadi zilizotokea katika serikali ya kaunti ya Nairobi alipokuwa mamlakani.

You can share this post!

Hisia mseto Wakenya wakiambiwa sasa barakoa si lazima

‘Polisi walioitisha hongo kwa sababu ya barakoa...

T L