• Nairobi
  • Last Updated March 5th, 2024 5:55 AM
Spika wa Bunge la Siaya akanusha njama ya kumng’oa Gavana Orengo licha ya duru kusema madiwani 30 ‘wameshaamua’

Spika wa Bunge la Siaya akanusha njama ya kumng’oa Gavana Orengo licha ya duru kusema madiwani 30 ‘wameshaamua’

NA KASSIM ADINASI

SPIKA wa Bunge la Kaunti ya Siaya George Okode amekanusha kuwepo kwa njama yoyote ya kumbandua Gavana James Orengo.

Bw Okode alisema kwa sasa, hakuna mswada wala mipango ya aina hiyo katika bunge la kaunti, hivi sasa, akisema kwamba wanashirikiana vyema na ofisi ya gavana.

“Ninaweka wazi kwamba hakuna mpango wa kumng’oa gavana, Waziri wa Fedha wa Kaunti ya Siaya au afisa yeyote kwa sababu hatuna sababu ya kufanya hivyo. Hii haimaanishi kwamba hatuwezi, kwa sababu kubandua viongozi mamlakani ni njia inayotumika idadi hitajika inapopatikana,” akasema Bw Okode alipohutubia wanahabari.

Ingawa hivyo, duru za kuaminika zinasema kuna mpasuko miongoni mwa madiwani.

Kuna kundi la madiwani wanaounga mkono kutimuliwa kwa gavana Orengo huku wengine wakipinga.

Wanaotaka atimuliwe wameandaa mswada, duru zilisema.

Bw Okode anapinga, na kuongeza kwamba mnamo Jumatatu, Oktoba 23, 2023, gavana alikutana na madiwani kujadili maswala muhimu ya kaunti.

“Pia tutakutana na gavana mnamo Jumapili, Oktoba 29, 2023, kujadili namna ya kuimarisha maisha ya wakazi,” akaongeza.

[email protected]

  • Tags

You can share this post!

Maafisa waliokuwa mstari wa mbele Shakahola wakiri safari...

Wabunge wa Nairobi na Mlima Kenya wapinga kufurushwa kwa...

T L