• Nairobi
  • Last Updated April 26th, 2024 11:13 AM
Kenya inaongoza Afrika kwa ukarimu – Utafiti

Kenya inaongoza Afrika kwa ukarimu – Utafiti

Na BERNARDINE MUTANU

Wakenya ni miongoni mwa watu wakarimu zaidi ulimwenguni. Katika utafiti uliofanywa na shirika la Uingereza, Charities Aid Foundation, Kenya iliorodheshwa ya nane, kati ya mataifa 146 kwa ukarimu.

Baadhi ya masuala yaliyokuwa yakizingatiwa ni kusaidia mtu usiyemjua, kutoa fedha na kujitolea kuhudumu kwa manufaa ya jamii.

Kenya ni taifa la pekee barani Afrika lililoko katika orodha ya mataifa 10 ulimwenguni yaliyo na watu wakarimu zaidi.

Kulingana na ripoti hiyo asilimia 72 ya Wakenya huwa tayari kusaidia mtu wasiyemjua kwa wakati wowote, asilimia 46 walitoa pesa na asilimia 45 walitoa wakati wao kusaidia.

Data hiyo ilikusanywa katika mataifa 146 kote ulimwenguni mwaka wa 2017.

Kulingana na ripoti hiyo, watu zaidi wanafaa kutiwa moyo kusaidia. Kulingana na ripoti hiyo, raia wa mataifa yanayoendelea ndio yalikuwa na watu wengi zaidi (asilimia 54) waliosaidia watu wasiowajua.

Mataifa hayo ni yale yamo Oceonia (asilimia 65) na Afrika (asilimia 58) huku Ulaya ikiwa chini kabisa (asilimia 44).

Wengi wa wale waliosaidia mtu wasiyemjua ni kati ya miaka 30-49 na kufuatwa na wale wa miaka kati ya 15 na 29.

You can share this post!

Nyani anyang’anya mwanamke mtoto na kumuua!

Mchepuko wavuruga harusi siku ya mwisho

adminleo