• Nairobi
  • Last Updated April 26th, 2024 7:00 PM
Kenya yakataa kuandaa AFCON 2019 kutokana na viwanja duni

Kenya yakataa kuandaa AFCON 2019 kutokana na viwanja duni

Na GEOFFREY ANENE

KENYA haitaomba kuandaa mashindano yoyote ya kimataifa ya soka hadi wakati viwanja vyake vitakapokuwa viko katika hali nzuri, Shirikisho la Soka la Kenya (FKF) limesisitiza.

Rais wa FKF Nick Mwendwa amesema kwamba Shirikisho la Soka la bara Afrika (CAF) lilikuwa limeomba Kenya kuwazia uenyeji wa Kombe la Afrika (AFCON) mwaka 2019 baada ya kupokonya Cameroon haki za kuandaa kindumbwendumbwe hicho kutokana na hali ya salama na pia viwanja kutokuwa tayari.

Cameroon ilipokonywa uenyeji mnamo Novemba 30 wakati kamati kuu ya CAF ilikuwa na kikao chake jijini Accra, Ghana. Ombi lake la kuandaa mashindano haya yanayofanyika kila baada ya miaka miwili Septemba mwaka 2014 wakati CAF ilikuwa chini ya uongozi wa raia wa Cameroon, Issa Hayatou. Rais wa sasa wa CAF ni raia wa Madagascar, Ahmad Ahmad.

“Kenya haitaomba kuandaa mashindano makubwa hadi pale viwanja vitakuwa tayari, pengine mwaka 2020,” amesema Mwendwa. Mara ya kwanza Mwendwa alitoa tangazo hili ilikuwa Agosti 28 baada ya Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) kukataa ombi la Kenya kuwa mwenyeji wa Kombe la Afrika la Wanawake (AWCON) mwaka 2018 ambalo nusura Ghana ipokonywe. Wakati huo, Mwendwa aliapa FKF haitaomba uenyeji wa mashindano yoyote yakiwemo yale ya Afrika Mashariki na Kati (Cecafa).

You can share this post!

FKF yahamisha kambi ya Harambee Stars kutoka Ufaransa hadi...

Mtapokea mamilioni yenu Machi 2019, Harambee Stars yaambiwa

adminleo