• Nairobi
  • Last Updated April 26th, 2024 2:25 PM
Magari ya Probox sasa yapigwa marufuku ya uchukuzi wa umma

Magari ya Probox sasa yapigwa marufuku ya uchukuzi wa umma

Na LUCY MKANYIKA

IDARA ya Trafiki imepiga marukufu magari aina ya Probox na mengine madogo kutumika kwa uchukuzi wa umma nchini. 

Akiongea mjini Voi, Kamanda wa Trafiki, Bw Samuel Kimaru alisema magari hayo yanafanya biashara ya kusafirisha umma kinyume cha sheria.

Bw Kimaru aliwaamuru wakuu wa trafiki katika kaunti mbalimbali kuhakikisha kuwa magari hayo yameondolewa barabarani haraka iwezekanavyo.

“Madereva wa magari hayo wana tabia ya kuendesha magari kwa kasi bila kujali maisha ya abiria. Oparesheni hii inafaa kuanza mara moja,” akasema.

Aliwataka wenye magari hayo kufanya biashara ya teksi badala ya uchukuzi wa umma.

Pia aliwaonya waendeshaji bodaboda wanaochukua sheria mikononi kuwa watachukuliwa hatua kali za kisheria.

Alisema kuwa wahudumu hao wamekuwa na tabia ya kuchoma magari yanayohusika katika ajali na wenzao.

“Tutakabiliana nao vikali. Uchomaji wa mali ni kosa kubwa sana kisheria na Hatutakubali makundi kama haya kuvunja sheria,” alisema.

You can share this post!

Fundi adai Sh195 milioni za kiti kilichokaliwa na Mzee Moi...

Achoma nyumba ya mpangaji kwa kutolipa kodi ya Sh2,000

adminleo