• Nairobi
  • Last Updated April 27th, 2024 8:03 AM
Video za ngono zihalalishwe mitandaoni – AKS

Video za ngono zihalalishwe mitandaoni – AKS

Na CHARLES WASONGA

CHAMA cha Wasiomwamini Uwepo wa Mungu Nchini (AKS) kimepuuzilia mbali mswada unaoharamisha usambazaji wa video, picha na jumbe chafu za ngono mitandaoni kikisema hatua hiyo haitakomesha uovu huo.

Kwenye taarifa Jumatatu mwenyekiti wa chama hicho Harrison Mumia alisema kuharamishwa kwa picha hizo kutachangia ongezeko la visa vya kuendeshwa kwa uovu huo kisiri.

“Tunapinga mswada huu wa marekebisho ya sheria kuhusu uhalifu wa mitandaoni. Bw Duale anaongozwa na chuki za kidini anapopendekeza mswada huu,” akasema.

Mbunge huyo wa Garissa ndiye mdhamini wa mswada huo ambao unatarajiwa kusomwa kwa mara ya kwanza bungeni katikati mwa wiki hii.

Kulingana na mswada huo, yeyote atakayepatikana akisambaza video, picha au jumbe za ngono atakuwa ameshiriki uhalifu na anaweza kutozwa faini ya hadi Sh20 milioni au kifungo cha miaka 25 gerezani, au adhabu zote mbili.

“Mtu hapaswi kuchapisha kwa njia ya kompyuta au kusambaza picha au video za kingono mitandao, au chombo chochote cha kupitisha habari, kimakusudi,” kielelezo cha mswada huo kinasema.

Kulingana na ASK watu wazima wako na haki ya kutizama video za ngono faraghani manyumbani mwao na hawafai kudhibitiwa kwa njia yoyote.

Bw Mumia alisema hatua bora ya kuzuia vijana kuathiriwa na mwenendo huo ni kuwapa elimu kuhusu masuala ya ngono tangu wakiwa wadogo.

Hata hivyo, Katibu Mkuu wa Muungano wa Wafanyakazi Nchini (COTU) Francis Atwoli amechangamkia mswada huo akisema utachangia kuendelezwa kwa maadili miongoni mwa wafanyakazi.

“Kando na maadili, kuzima kwa uovu huo utawahakikishia usalama wao wafanyakazi, vijana na wanajamii kwa ujumla ambao huathiriwa na uovu huu mitandaoni,” akasema Bw Atwoli kwenye taarifa kwa vyombo vya habari.

You can share this post!

TAHARIRI: Mswada wa Duale usipingwe ovyo

Diwani ang’olewa uongozini kutokana na hongo