Ramaphosa aitaka Afrika ijitengenezee chanjo ya corona

Na AFP

RAIS wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amesisitiza kuwa Afrika inahitaji ujuzi na uwezo wa kuunda chanjo zake binafsi.

Alisema hayo wakati bara la Afrika linashikilia mkia miongoni mwa maeneo mengine ulimwenguni katika mchakato wa kupeana chanjo dhidi ya Covid-19.

Huku ikiwa imetoa asilimia mbili pekee ya jumla ya chanjo zote zilizotolewa kote ulimwenguni, “Afrika inahitaji kujiimarisha binafsi kama bara na kutambua nafasi za ushirikiano na mataifa mengine,” alisema Ramaphosa.

Alisema hayo kwenye kongamano kuhusu uundaji wa chanjo, lililoandaliwa na Vituo vya Afrika kuhusu Kudhibiti na Kuzuia Maradhi (Africa CDC) mnamo Jumatatu.

Alisema mataifa mengine nje ya bara hili yanaweza “yakatoa ujuzi wa kiufundi, kifedha na uwekezaji.”

Alipendekeza kuwa India na Brazil zinaweza kusaidia katika kutoa mwongozo kuhusu jinsi zilivyoanzisha kampuni zao binasfi za kutengeneza dawa.

“Tunahitaji vilevile kujiimarisha kupitia uhamishaji wa ujuzi na maarifa ili kuhakikisha tunaweza kustawisha uzalishaji nchini,” alisema Ramaphosa.

 

Habari zinazohusiana na hii