• Nairobi
  • Last Updated April 26th, 2024 3:03 PM
KNUT: Walalama Sossion amesambaratisha chama

KNUT: Walalama Sossion amesambaratisha chama

Na TITUS OMINDE

MGAWANYIKO unaendelea kutikisa chama cha Walimu nchini Knut huku uchaguzi wa kitaifa ukitarajiwa kufanyika Juni 20.Kambi mbili zinazoongozwa na Katibu Wilson Sossion na kaimu mwenyekiti wa Kitaifa, Bw Collins Oyuu, zinazidi kutupiana cheche za maneno uchaguzi huo ukikaribia.

Kikosi cha Bw Oyuu kinadai kuwa Bw Sossion amesambaratisha chama hicho.Bw Oyuu alimkashfu Bw Sossion kwa kudunisha maafisa wengine wa Knut kwa kuendesha shughuli za muungano huo kama mali ya mtu binafsi.

“Ubinafsi na udikteta wa Bw Sossion umeua umoja wetu. Amechukua Knut kama mali ya kibinafsi. Anafanya maamuzi ya chama bila kushauriana na viongozi wengine,” alisema Bw Oyuu.

Akiongea mjini Eldoret mnamo Ijumaa wakati wa mkutano na wajumbe wa Knut Rift Valley, Bw Oyuu alisema changamoto za sasa zinazotishia kuvunjika kwa Knut zinatokana na utawala mbaya wa Bw Sossion.

Bw Oyuu alisema kuondolewa kwa Bw Sossion kutoka kwa uongozi wa Knut kutaashiria hatima ya umoja wa Knut chama ambacho awali kilikuwa kikijivunia kuwa na halaiki ya wanachama ambao ni walimu na kutetemesha serikali.

You can share this post!

JAMVI: Mwaura alivyojikwaa na kujiponza kisiasa

JAMVI: ‘Baba’ anajua kwamba UhuRuto wanamkata...