• Nairobi
  • Last Updated April 26th, 2024 3:10 PM
Celtic waajiri kocha Ange Postecoglou kujaza pengo la Neil Lennon

Celtic waajiri kocha Ange Postecoglou kujaza pengo la Neil Lennon

Na MASHIRIKA

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

ANGE Postecoglou, 55, ameteuliwa kuwa kocha mpya wa klabu ya Celtic ili kujaza pengo la Neil Lennon aliyejiuzulu mnamo Februari 2021 baada ya kikosi hicho kushindwa kushinda taji la Ligi Kuu ya Scotland kwa mara ya 10 mfululizo.

Postecoglou ambaye ni kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Australia, anatua Celtic kwa mkataba wa miezi 12 baada ya kukatiza uhusiano wake na klabu ya Yokohama F Marinos.“Nitafanya kila linalowezekana kurejesha uthabiti wa kikosi hiki. Tunalenga kufurahisha mashabiki wetu pamoja na kutia kapuni mataji ya haiba,” akasema kocha huyo mzawa wa Ugiriki.

Celtic walishawishika kumuajiri Postecoglou baada ya Eddie Howe kukataa fursa ya kuhamia jijini Glasgow kwa sababu ambazo alisema “ziko nje ya uwezo wake kudhibiti”.Kwa kuwa Postecoglou atatakiwa kujitenga kwa siku 10, ina maana kwamba atakosa vipindi kadhaa vya mwanzo wa kujiandaa kwa msimu mpya wa 2021-22.

Hivyo, mchuano wake wa kwanza kusimamia kambini mwa Celtic ni wa kufuzu kwa soka ya Klabu Bingwa Ulaya (UEFA) mnamo Julai 2021.Postecoglou aliwahi kushinda mataji mawili ya Ligi Kuu ya Australia (A-League) akidhibiti mikoba ya kikosi cha Brisbane Roar kabla ya kuhamia kambini mwa Melbourne Victory na hatimaye kuwa kocha wa timu ya taifa ya Australia mnamo 2013.

Aliongoza Australia kufuzu kwa fainali a Kombe la Dunia za 2014 na 2018 nchini Brazil na Urusi mtawalia kabla ya kuhamia Japan mnamo 2017 kudhibiti mikoba ya Yokohama waliotawazwa mabingwa wa Ligi Kuu (J-League) mnamo 2019.Postecoglou ambaye ni kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Australia, anatua Celtic kwa mkataba wa miezi 12 baada ya kukatiza uhusiano wake na klabu ya Yokohama F Marinos.

ANGE Postecoglou, 55, ameteuliwa kuwa kocha mpya wa klabu ya Celtic ili kujaza pengo la Neil Lennon aliyejiuzulu mnamo Februari 2021 baada ya kikosi hicho kushindwa kushinda taji la Ligi Kuu ya Scotland kwa mara ya 10 mfululizo.

“Nitafanya kila linalowezekana kurejesha uthabiti wa kikosi hiki. Tunalenga kufurahisha mashabiki wetu pamoja na kutia kapuni mataji ya haiba,” akasema kocha huyo mzawa wa Ugiriki.Celtic walishawishika kumuajiri Postecoglou baada ya Eddie Howe kukataa fursa ya kuhamia jijini Glasgow kwa sababu ambazo alisema “ziko nje ya uwezo wake kudhibiti”.

Kwa kuwa Postecoglou atatakiwa kujitenga kwa siku 10, ina maana kwamba atakosa vipindi kadhaa vya mwanzo wa kujiandaa kwa msimu mpya wa 2021-22. Hivyo, mchuano wake wa kwanza kusimamia kambini mwa Celtic ni wa kufuzu kwa soka ya Klabu Bingwa Ulaya (UEFA) mnamo Julai 2021.

Postecoglou aliwahi kushinda mataji mawili ya Ligi Kuu ya Australia (A-League) akidhibiti mikoba ya kikosi cha Brisbane Roar kabla ya kuhamia kambini mwa Melbourne Victory na hatimaye kuwa kocha wa timu ya taifa ya Australia mnamo 2013.

Aliongoza Australia kufuzu kwa fainali a Kombe la Dunia za 2014 na 2018 nchini Brazil na Urusi mtawalia kabla ya kuhamia Japan mnamo 2017 kudhibiti mikoba ya Yokohama waliotawazwa mabingwa wa Ligi Kuu (J-League) mnamo 2019.

 

  • Tags

You can share this post!

Wakulima wahimizwa kukumbatia kilimo cha maparachichi ya...

Barabara zafungwa jijini bajeti ikisomwa