Bajeti 2021/2022: Michezo ya kamari kutozwa ushuru wa asilimia 20

Na SAMMY WAWERU

IMEKUWA pigo tena kwa waraibu wa michezo ya kamari baada ya serikali kutangaza kuanza kuitoza ushuru. 

Mwaka uliopita, Rais Uhuru Kenyatta alitia saini mswada wa kuondoa ushuru kwa michezo hiyo. Kabla ya hatua ya rais, baadhi ya kampuni na mashirika ya kamari, kama vile Sportpesa na Bettin, nchini yalikuwa yamesitisha ufadhili wake kwa vilabu vya soka.

Kwenye Makadirio ya Bajeti Mwaka wa Fedha 2021/2022, serikali imetangaza kuwa michezo hiyo itakuwa ikitozwa ushuru wa asilimia 20.  “Ushuru wa asilimia 20 kwa michezo ya kamari umerejeshwa,” akasema Waziri wa Fedha na Hazina ya Kitaifa, Balozi Ukur Yattani.

Baadhi ya wakosoaji wamekuwa wakitaka michezo ya kamari kupigwa marufuku nchini, wakiitaja kuwa kichocheo cha vijana kupotoka.