• Nairobi
  • Last Updated April 26th, 2024 5:10 PM
Waziri atangaza Sikukuu Jumanne Waislamu wakiadhimisha Idd-ul-Adha

Waziri atangaza Sikukuu Jumanne Waislamu wakiadhimisha Idd-ul-Adha

Na MARY WANGARI

WAISLAMU watasherehekea Sikukuu ya Idd-ul-Adha Jumanne baada ya Waziri wa Usalama wa Ndani, Dkt Fred Matiang’i kutangaza siku hiyo kuwa sikukuu ya kitaifa.

Kupitia notisi rasmi iliyochapishwa jana katika gazeti la serikali, waziri Matiang’i alitangaza Jumanne siku ya kuadhimisha mwisho wa Haji, ambayo ni safari ya waumini wa Kiislamu kwenda kuhiji Mecca.

“Umma unafahamishwa kwamba kuambatana na mamlaka aliyotwikwa na Sheria kuhusu Sikukuu za Umma, Waziri wa Usalama wa Ndani anatangaza Jumanne, Julai 20 kuwa siku ya kuadhimisha siku kuu ya Idd-Ul-Adha, 2021,” ilisema notisi hiyo.

Haya yamejiri miezi michache tu baada ya Baraza Kuu la Waislamu Nchini kuwasilisha ombi siku hiyo kutangazwa rasmi kama sikukuu.

“Kile ambacho kimeruhusiwa tangu enzi za rais wa kwanza Jomo Kenyatta ni Eid ul Fitr lakini inapohusu Eid al-Adha serikali imekuwa ikituchezea. Wakati mwingine huwa wanatoa notisi, tunachoshinikiza ni kwamba siku hii kutangazwa sikukuu kikamilifu,” alisema Mkurugenzi wa Supkem, Sheikh Hassan Kinyua, awali.

You can share this post!

ODM yataka msajili atatue mzozo wa fedha wa NASA

Mganga ataka shirika limrejeshee Sh18.5m