Rais abadilisha simu baada ya jaribio la wadukuzi dhidi yake

RAIS wa Ufaransa Emmanuel Macron alibadilisha simu na nambari yake baada ya ripoti kumfikia kwamba analengwa na wadukuzi wa mitandao wa Israeli maarufu kama Pegasus.

Ofisi ya Rais pia ilisema kwamba Macron aliagiza mabadiliko katika mipango ya usalama wake.

Mnamo wiki hii, gazeti la Le Monde liliripoti kwamba mawaziri 14 wa ufaransa walikuwa wakifuatiliwa na wadukuzi wa Morocco.

Maafisa wa serikali ya Morocco wamekanusha kwamba wamekuwa wakitumia vifaa vya udukuzi kutoka Israeli na kwamba madai hayo ni ya uongo wala hayana msingi.

Israeli ina vifaa vinavyoweza kuvizia simu na tarakilishi na kutwaa habari za watu zikiwemo jumbe, picha na barua pepe.

Haikubainika iwapo iliweka kifaa hicho ikilenga Ufaransa na hasa simu ya Macron lakini nambari yake ina orodha ya watu 50,0000 ambao, inaaminika, wanalengwa na wateja wa NSO Group, waliobuni Pegasus mwaka wa 2016.

Kifaa hicho kina uwezo wa kufanya ujasusi wa mtandao kwa kunasa mawasiliano ya simu na tarakilishi.

Imeripotiwa kwamba wengine wanaolengwa ni marais Baram Salih wa Iraq, Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini na mawaziri wakuu wa Pakistan,Misri na Morocco.