ULIMBWENDE: Tengeneza maski ya nywele kwa kutumia ‘sour cream’

Na MARGARET MAINA

mwmaina@ke.nationmedia.com

BIDHAA kama sour cream inajulikana na inapendwa na watu wengi kwa sababu inaongeza ladha kwa vyakula ikitumika jikoni.

Mbali na lishe inaweza kutumiwa kama kipodozi na baadhi ya wanawake hutumia kuhifadhi uzuri na afya ya nywele na ngozi.

Ukiitumia mara kwa mara inaweza kukupa matokeo mazuri na kudumisha matokeo haya kwa muda mrefu.

Maski ya bidhaa hii inaweza kutumika usoni. Lakini muhimu zaidi ni ikitumika kwa nywele.

Sour cream kwa nywele kavu

Maski nzuri kwa aina ya nywele kavu, inatengenezwa kwa kuchanganya asali, sour cream, yai na viazi vibichi.

Chukua viazi vidogo, vichambue na ukwangue halafu ongeza kijiko cha sour cream na ute wa yai.

Vyote hivi changanya kwa makini na upake kwa ngozi usoni na kichwani na uache kwa muda wa dakika 20-25.

Funika kichwa chako kwa kitambaa kikubwa kisha baada ya muda osha nywele zako kwa shampoo (ambayo unatumia kila wakati).

Changanya vijiko viwili vya sour cream, ongeza na viini viwili vya mayai ili kuimarisha nywele na kutoa ‘lishe’ nzuri kwa nywele.

Siki hii ni muhimu kwa uzuri na afya kwa sababu ina seti kubwa ya vitamini, protini, asidi na sukari.

Matumizi ya nje ya sour cream kwa nywele

  • nywele hupata protini na vitu vyote muhimu,
  • huimarisha mizizi na mwili wa nywele,
  • inaboresha sana muonekano,
  • inachangia ukuaji wa kawaida na uimarishaji wa nywele.