• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 12:48 PM
3 kizimbani kwa madai ya wizi wa pembe za ndovu

3 kizimbani kwa madai ya wizi wa pembe za ndovu

NA ALEX KALAMA

WANAUME watatu wamefikishwa katika Mahakama ya Malindi kwa mashtaka ya kuhusika na wizi wa pembe za ndovu.

Samson Mweri Jefwa, Karisa Kilemba Mburo na Kazungu Katana Samwel walikana mashtaka mbele ya Hakimu Mkuu wa Malindi, Bi Elizabeth Usui.

Inadaiwa kuwa Juni 5 walipatikana eneo la Marereni-Kibaoni katika Kaunti ndogo ya Magarini, Kaunti ya Kilifi walipatikana wakiuza viungo vya wanyamapori ambayo ni vipande vitano vya pembe za ndovu vyenye uzani wa kilo 21 na thamani ya shilingi laki tano.

Hata hivyo inadaiwa walikuwa wakitekeleza biashara hiyo kinyume cha sheria za Kenya kwani hawakuwa na kibali kutoka kwa mkurugenzi mkuu shirika la huduma kwa wanyama pori (KWS).

Kifungu cha 92 (2) cha Sheria ya Usimamizi wa Uhifadhi wa Wanyamapori ya mwaka 2013 kinaharamisha kujihusisha na biashara ya wanyamapori na kosa hilo linaweza kuvutia kifungo cha chini cha miaka 15 jela na kisichopungua shilingi milioni moja faini.

Usui aliamuru washtakiwa warudishwe rumande katika gereza la Malindi Mtangani baada ya kushindwa kulipa dhamana ya shilingi laki tano kila mmoja huku kesi hiyo ikitajwa tena Juni 21, 2022.

  • Tags

You can share this post!

Austria ya kocha Ralf Rangnick yaendeleza masaibu ya...

Raila atuma Karua ngome ya Ruto

T L