• Nairobi
  • Last Updated May 19th, 2024 9:01 PM
Austria ya kocha Ralf Rangnick yaendeleza masaibu ya Ufaransa katika Nations League

Austria ya kocha Ralf Rangnick yaendeleza masaibu ya Ufaransa katika Nations League

Na MASHIRIKA

KYLIAN Mbappe alisaidia Ufaransa kuzoa alama moja dhidi ya Austria baada ya kusawazishia mabingwa hao wa dunia dakika za mwisho kwenye sare ya 1-1 katika gozi la Uefa Nations League mnamo Ijumaa.

Mbappe aliyetokea benchi katika kipindi cha pili, alifunga bao la kusawazisha katika dakika ya 83 na kufuta juhudi za fowadi wa Bristol City, Andreas Weimann, aliyewaweka Austria kifua mbele kunako dakika ya 37. Bao hilo la Weimann, 30, lilikuwa lake la kwanza kimataifa.

Kufikia sasa, Ufaransa wana alama mbili pekee kutokana na mechi tatu za Kundi A1. Mambo yangewaendea mrama zaidi iwapo Weimann, aliyefunga mabao 22 katika Ligi ya Daraja ya Kwanza nchini Uingereza (Championship) msimu huu angepachikia Austria goli la pili mwishoni mwa kipindi cha pili.

Karim Benzema alipoteza nafasi nyingi za wazi dhidi ya Austria ambao sasa wanatiwa makali na aliyekuwa kocha mshikilizi kambini mwa Manchester United, Ralf Rangnick.

Kipa Patrick Pentz alifanya pia kazi nyingi ya ziada na kunyima Christopher Nkunku, Matteo Guendouzi na Mbappe nafasi za kufungia Ufaransa bao la ushindi.

Ufaransa walianza kampeni zao za Kundi A1 kwa kichapo cha 2-1 dhidi ya Denmark kabla ya kutoka sare ya 1-1 dhidi ya Croatia. Sasa wanavuta mkia kwa pointi mbili, nne nyuma ya viongozi Denmark na mbili nyuma ya Croatia na Austria. Croatia walivuna ushindi wao wa kwanza kundini Ijumaa baada ya kutandika Denmark 1-0.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Kesi ya Sonko na IEBC kuhusu idhini ya kuwania ni wiki ijayo

3 kizimbani kwa madai ya wizi wa pembe za ndovu

T L