• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 5:40 PM
Kaluma afurahia kutiwa saini kwa mswada wa kuzima ‘mpango wa kando’ katika urithi

Kaluma afurahia kutiwa saini kwa mswada wa kuzima ‘mpango wa kando’ katika urithi

Na CHARLES WASONGA

MBUNGE wa Homa Bay Mjini Peter Kaluma Jumatano alijawa na furaha baada ya Rais Uhuru Kenyatta kutia saini mswada wa marekebisho ya sheria ya urithi aliyodhamini bungeni mnamo 2019.

Mswada huo ambapo unawazima wapenzi wa kisiri kurithi mali ya mtu anapofariki sasa ni sheria kufuatia sahihi hiyo ya kiongozi wa taifa.

Kwa mahojiano na Taifa Leo Jumatano jioni, Bw Kaluma alisema kutiwa saini kwa mswada huo ni ushindi mkubwa kwa wanaume na pigo kubwa kwa wapenzi hao, maarufu kama “mipango ya kando” au “slay queens” ambao hutokea na kudai wagawiwe mali ya wanaume waliofariki. Hii ni licha ya kwamba hawakuwa katika uhusiano halali wa ndoa na wanaume hawa walipokuwa hai.

Kumekuwa na visa vingi vya familia ya wanaume, haswa matajiri au watu wenye ushawishi wa kisiasa, kuhangaishwa na wanawake wanaodai mali kwa misingi kuwa walipata watoto katika mahusiano yao (haramu).

“Leo ni siku ya furaha kuu kwangu kama mbunge. Matapeli ambao wamekuwa wakivizia mali ya wafu wamezimwa. Ni wale walioko katika ndoa halali inayotambuliwa chini ya Sheria ya Ndoa ndio sasa watarithi mali ya marehemu,” Bw Kaluma akaongeza.

Alisema sheria hiyo inalinda watoto wa mwendazake pekee na wala sio wanawake ambao hutokea na kudai mali.

“Lakini ningetaka ieleweke kuwa watoto wa marehemu aliopata na mkewe wa ndoa au mpenzi wake wa kando wamelindwa na sheria hii. Watoto wote wa mwanamume aliyefariki watapata urithi wa mali yake,” Bw Kaluma, ambaye ni mwanasheria, alisema.

  • Tags

You can share this post!

Mahakama yakubali ushindi wa marehemu Jeniffer Wambua...

Mshukiwa katika kesi ya Obado ajifungua huku bintize...

T L