• Nairobi
  • Last Updated April 28th, 2024 4:55 PM
Akamatwa na bastola feki na kutupwa jela

Akamatwa na bastola feki na kutupwa jela

Na RICHARD MUNGUTI

MSHUKIWA wa ujambazi aliyekamatwa na bastola feki aliyokuwa anatumia kutisha wananchi ameshtakiwa kujiandaa kutekeleza uhalifu.

Gilbert Ochieng aliye na umri wa miaka 41 alishtakiwa kujiandaa kutekeleza uhalifu wa wizi wa mabavu. Ochieng alitiwa nguvuni katika barabara ya Ole Sereni karibu na chuo kikuu cha Strathmore University mnamo Oktoba 14, 2021.

Baadhi ya wananchi waliotishwa na mshtakiwa waliwapasha polisi habari hizo. Mshtakiwa alikamatwa na bastola  hiyo bandia ikakutwa ameificha kibidoni. Polisi waliomkamata mshtakiwa walikuwa wanalinda jengo la serikali.

Alizuiliwa katika kituo cha polisi cha Langata. Mshtakiwa alimsihi hakimu mkazi Charles Mwaniki amwachilie kwa dhamana. Hakimu aliamuru mshtakiwa azuiliwe gerezani hadi Novemba 3, 2021 ripoti ya afisa wa urekebishaji tabia itakapowasilishwa ili ibainike endapo ataachiliwa kwa dhamana.

 

  • Tags

You can share this post!

Refarii Omagwa ajiwekea malengo ya kufika mbali katika soka

Awara amlewesha Mganda na kumpora Sh130,000

T L