• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 2:31 PM
Aliyejaribu kuua polisi kukaa gereza la viwandani

Aliyejaribu kuua polisi kukaa gereza la viwandani

Na RICHARD MUNGUTI

MFANYABIASHARA anayeshtakiwa kujaribu kuwaua maafisa wa wawili wa polisi na weita atazuiliwa katika gereza la viwandani hadi Agosti 5,2021 mahakama itakapo mweleza masharti ya kuachiliwa kwa dhamana.

Hakimu mwandamizi Bi Esther Kimilu aliamuru Dickson Njanja Mararo azuiliwe katika gereza la viwandani upande wa mashtaka uweke mipango kabambe ya kuwalinda mashahidi wanaodaiwa maisha yao yako hatarini.Bi Kimilu aliyesema atamwachilia mshtakiwa kwa dhamana mnamo Agosti 5, 2021 alisema upande wa mashtaka wahitaji kupewa fursa ya kukamilisha masuala kadhaa kabla ya mshtakiwa kutangaziwa masharti yake ya dhamana.

Akitoa uamuzi wa dhamana , Bi Kimilu alisema dhamana ni haki ya kila mshukiwa anayeshtakiwa mahakamani.“Nimetilia maanani mawasilisho ya wakili Cliff Ombeta pamoja na yale ya kiongozi wa mashtaka Bi Everlyn Onunga na kufikia uamuzi mshtakiwas yafaa aachiliwe kwa dhamana,” Bi Kimilu alisema.

Hakimu huyo alisema upande wa mashtaka wahitaji kupewa fursa ya kuwahifadhi mashahidi wanaohofia maisha yao.Akipinga mshtakiwa akiachiliwa kwa dhamana Bi Onunga alisema mlalamishi Festus Musyoka Kavuthi angali hali mahututi.

“Kavuthi angali amelazwa Nairobi Hospital. Bado hajaaza kuzugumza kutokana na majeraha aliyopata,” alisema Bi Onunga.Kiongozi huyo wa mashtaka alisema tayari bili ya hospitali imefika Sh4milioni.Wakili wa familia ya Kavuthi, Bw Daniel Maanzo , alipinga mshtakiwa akiachiliwa kwa dhamana.

Wakili Daniel Maanzo (kulia) azugumza na naibu wa mkurugenzi wa mashtaka ya umma Alexander Muteti Ijumaa katika mahakama ya Milimani…Picha/RICHARD MUNGUTI

“Hata mhasiriwa yuko na haki.Mshtakiwa hapasi kuachiliwa kwa dhamana kabla ya Kavuthi kuandikisha taarifa yake. Kavuthi angali amelazwa Nairobi Hospital.Amelemaa na hajaanza kunena,” Bw Maanzo alimjulisha hakimu.Akitoa uamuzi Bi Kimilu alisema mkurugenzi wa mashtaka ya umma anapasa kupewa muda kuwahifadhi mashahidi.

Aliamuru mshtakiwa azuiliwe kwa siku 14 zaidi katika gereza ka Viwandani hadi Agosti 5,2021.Dickson Njanja Mararo , ameshtakiwa kwa kujaribu kuwaua Festus Musyoka Kavuthi na Lawrence Muturi na weita katika kilabu cha mkahawa wa Quivers Lounge Bi Felistus Nzisa.

Alikanusha mashtaka hayo na kuomba aachiliwe kwa dhamana.Mararo alisema wazazi wake walienda kumwona Kavuthi hospitali na pia walienda kuwaona watu wa familia ya mhasiriwa huyo.Muturi na Nzisa aliyechapwa risasi ya tumbo walitibiwa na kuruhusiwa kwenda nyumbani.

Kavuthi alipigwa risasi shingoni na amelemaa.

  • Tags

You can share this post!

Mwitaliano ashtakiwa kuiba teksi

JAMVI: Gavana Kingi aning’inia kisiasa Muungano wa...