• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 8:55 PM
Aliyejifanya Mhindi Facebook ashtakiwa kwa ubakaji

Aliyejifanya Mhindi Facebook ashtakiwa kwa ubakaji

Na Richard Munguti

MWANAUME aliyebadilisha jina lake la Kiafrika katika mtandao wa Facebook na kujiita jina la Mhindi kisha akamdanganya mwanamke kutoka kaunti ya Meru atamwajiri kazi Nairobi alishtakiwa Ijumaa kwa ubakaji na wizi wa mabavu.

Bw Godfrey Maranga Nyakundi aliyejitambulisha katika mtandao wa Facebook kuwa Hanuman Hanuman na kumndanganya mwanamke atamwajiri kazi ya Supa alishtakiwa mbele ya hakimu mkuu mahakama ya Milimani Bi Martha Mutuku.

Bw Nyakundi alimaarufu Hanuman Hanuman alikabiliwa na mashtaka matatu ya wizi wa mabavu na dhuluma za kimapenzi.

Kiongozi wa mashtaka Bw Anderson Gikunda alimweleza Bi Mutuku mnamo February 4,2021 mlalamishi alifungua mtandao wa Facebook na kuona nafasi ya kazi imetangazwa na Hanuman (nyakundi).

Bw Nyakundi alimpigia simu mlalamishi na wakaelewana jinsi atasafiri kutoka Meru hadi Nairobi kuajiriwa kazi ya Supa.

Mlalamishi alielezwa atakuwa anapokea mshahara wa Sh18,000 kwa mwezi.

Bw Gikunda alisema mnamo Feburuari 8,2021 mlalamishi alisafiri kutoka Meru kukutana na mshtakiwa Nairobi.

Alipowasili mlalamishi alikutana na mshtakiwa.

“Mshtakiwa alimpeleka mlalamishi katika makazi yake mtaani Kibra kisha akamnyang’anya simu yake muundo wa Infinix Smart 4 yenye thamani ya Sh16,000,” Bw Gikunda alieleza mahakama.

Mshtakiwa alikanusha mashtaka kisha akaomba aachiliwe kwa dhamana.

Bw Gikunda hakupomga ila alieleza korti izingatie ukali wa mashtaka na adhabu atakayopata mshtakiwa akipatikana na hatia.

Bi Mutuku alimwachilia kwa dhamana ya Sh500,000 na mdhamini mmoja ama alipe pesa tasilimu Sh300,000 ndipo aachiliwe kutoka kizuizini.

Kesi itatajwa baada ya wiki mbili.

  • Tags

You can share this post!

Wachuuzi wa ahadi hewa

Polisi kukamatwa kwa kutofika kortini