• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 5:50 AM
Aliyepokea 162,000 kimakosa akanunua ploti ajipata taabani

Aliyepokea 162,000 kimakosa akanunua ploti ajipata taabani

Na RICHARD MUNGUTI

FUNDI stima aliyepokea zaidi Sh162,000 katika mtandao wake wa M-Pesa zilizotumwa kimakosa kwa simu yake kutoka kwa Benki ya Cooperative ameomba kaunti ya Migori ameomba mahakama apewe muda azilipe kwa kiwango cha Sh1,000 kila mwezi.

Stephen Nyamwita John aliyekiri kupokea pesa hizo mnamo Februari 15,2023 alimsihi hakimu mkuu mahakama ya Milimani Nairobi Lucas Onyina arudishwe nyumbani Migori anakofanya kazi ya stima apate kuuza shamba arudishe pesa hizo.

“Ni ukweli nilipokea pesa hizi Sh162,120. Nilizitumia kununua shamba. Naomba nipewe muda nimtafute mnunuzi niliuze tena nizirudishe kwa Benki ya Cooperative,” Nyamwita alimsihi Bw Onyina.

Nyamwita aliye na umri wa miaka 27, 2023 alikiri shtaka la kuhifadhi kimakosa pesa zisizo zake.

Pesa hizo zilitumwa kutoka kwa akaunti ya kampuni ya Pan African Network Group iliyoko Benki ya Cooperative Migori.

Mshtakiwa alipokea pesa hizo katika eneo la Mabera iliyoko kaunti ya Migori.

Bw Onyina aliamuru idara ya urekebishaji tabia iwasilishe ripoti ya mshtakiwa na jamaa zake kabla kumwadhibu.

Nyamwita aliyeonyesha unyenyekevu akiomba apewe muda wa kurudisha pesa hizo aliamriwa azuiliwe katika gereza lililoko eneo la Viwandani hadi Aprili 3, 2023.

  • Tags

You can share this post!

Wafuasi wa Azimio Kilifi wataka Mnyazi, Chonga na Madzayo...

Raila asema hatachoka kudai haki na kupigania maisha bora...

T L