• Nairobi
  • Last Updated February 22nd, 2024 1:05 PM
Ashtakiwa kwa kulaghai mke wa rafikiye Sh2 milioni

Ashtakiwa kwa kulaghai mke wa rafikiye Sh2 milioni

Na RICHARD MUNGUTI

MUUZAJI mashamba na ardhi ameshtakiwa kwa kumlaghai mke wa rafikiye anayeishi Amerika Sh2 milioni.

Esrom Kamande Kamau mwenye umri wa miaka 42 alikabiliwa na shtaka la kumlaghai Jacinta Wangari Kimotho Sh2, 097, 680 akidai atamuuzia shamba katika mtaa wa Thome eneo la Kasarani, Nairobi.

Alipotunguliwa pesa hizo Wangari alikuwa anaugua.

Esrom amekana kumlaghai Wangari pesa hizo kati ya Septemba 25, 2020 na Aprili

15, 2023.

Mahakama ilielezwa kuwa mshtakiwa alishirikiana na watu wengine ambao hawakufikishwa kortini kutekeleza uhalifu huo.

Mshtakiwa alikana shtaka mbele ya hakimu mwandamizi Hellen Onkwani na kuachiliwa kwa dhamana.

Kesi itaanza kusikizwa Novemba 11, 2023.

  • Tags

You can share this post!

Mahabusu aliyegeuza seli kuwa uwanja wa ndondi aona moto

Atishia kuua mpangaji kwa kunyimwa ‘tunda la ndoa’

T L