• Nairobi
  • Last Updated May 22nd, 2024 5:30 PM
Atishia kuua mpangaji kwa kunyimwa ‘tunda la ndoa’

Atishia kuua mpangaji kwa kunyimwa ‘tunda la ndoa’

Na RICHARD MUNGUTI

MWANAUME aliyenyimwa tendo la ndoa na mpangaji katika jengo la wazazi wake ameshtakiwa kwa kutisha kumuua mwanadada huyo.

Ian Mutwii Mwenga alishtakiwa mbele ya hakimu mkazi Mercy Malingu kwa kumtumia ujumbe wenye vitisho mlalamishi mnamo Mei 21, 2023.

Mshtakiwa alidaiwa alimtumia ujumbe mlalamishi uliosema “we tafuta nyumba ingine mapema nimekupea hii mwezi pekee, kama si hivyo utazikwa mbila kichwa.”

Upande wa mashtaka ulisema mlalamishi alieleza polisi mshtakiwa amekuwa akimtaka washiriki tendo la ngono kisha akakataa.

Mshtakiwa alikana shtaka na kuachiliwa kwa dhamana ya Sh200, 000.

Kesi itasikizwa Novemba 1, 2023.

  • Tags

You can share this post!

Ashtakiwa kwa kulaghai mke wa rafikiye Sh2 milioni

Kisumu All Starlets kukwaana na Ulinzi Starlets kwenye...

T L