• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 11:53 AM
BrighterMonday yazindua teknolojia ya kuwasaidia waajiri kupata wafanyakazi bora

BrighterMonday yazindua teknolojia ya kuwasaidia waajiri kupata wafanyakazi bora

NA WINNIE ONANDO

JUKWAA la mtandao la kuchapisha nafasi za kazi la BrighterMonday, limezindua teknolojia mpya inayowasaidia waajiri kupata wafanyakazi bora walio na tajriba na uwezo wa kuimarisha na kufanikisha biashara na kampuni zao.

Teknolojia hiyo mpya inasaidia kupunguza muda wanaochukua waajiri kupata wafanyakazi waliohitimu.

Haya yanafuata mabadiliko na uvumbuzi mbalimbali katika sekta ya ajira.

Teknolojia hiyo mpya hurahisisha mchakato wa kuajiri kwa gharama nafuu kwa wakati unaofaa zaidi ikilinganishwa na mbinu za jadi za kuajiri.

Kadhalika, itasaidia kuokoa muda na pesa wanazotumia waajiri hasa katika kuwachuja wanaotafuta kazi jambo ambalo linapunguza muda unaochukuliwa kwa mchakato wa kuajiri.

Kwa jumla, waajiri wataweza kupata wafanyakazi bora wenye tajriba wanaohitaji katika kampuni au biashara lengwa.

Uzinduzi huo unakuja wiki chache baada ya jukwaa hilo kutangazwa kuwa maarufu na lenye kupendelewa na mamilioni ya wanaotafuta ajira.

Akizungumza mwishoni mwa mwezi Mei, mkuu wa idara ya mauzo katika kampuni hiyo Erick Wilson Wafula alisema kuwa, kampuni hiyo itaendelea kupanua huduma zake ili kuleta pamoja watu wengi zaidi wanaotafuta ajira na waajiri.

“Tuna uwezo wa kuwezesha waajiri kupata watu waliona tajriba hitajika ili kuboresha sekta ya ajira nchini. Waajiri watapata orodha ya majina ya watu waliobobea katika sekta hitajika. Hii itawawezesha kuwaajiri watu waliona uwezo wa kuwasaidia kuendeleza na kuimarisha kampuzi zao,” akasema Bw Wafula

  • Tags

You can share this post!

DOMO: Walichomea picha shangazi Riri!

Mwanadada ashtakiwa kuiba saa na simu ya mpenziwe

T L