• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 5:50 AM
CDF: Wabunge sasa watishia kususia kazi

CDF: Wabunge sasa watishia kususia kazi

Wabunge zaidi ya 300 leo Jumatatu wametishia kusitisha shughuli za bungeni hadi Wizara ya Fedha itakapowapa fedha za Hazina ya Kitaifa ya Kistawisha Maendeleo (NG-CDF).

Serikali ya kitaifa hutegemea bunge kupitisha sera na sheria mbalimbali ambazo ni muhimu kwa utekelezaji wa huduma na maendeleo ya kitaifa.

Leo Jumatatu, wabunge hao wamesitisha mkutano wao wa wiki moja katika hoteli ya kifahari ya Pride Inn Paradise iliyo Kaunti ya Mombasa wakilalamikia kuwa CDF imecheleweshwa.

Wakiongozwa na mwenyekiti wa kamati ya hazina hiyo, Bw Musa Sirma, ambaye ni Mbunge wa Eldama Ravine, walisema wabunge wanafaa kupewa Sh12 bilioni za CDF kulingana na ahadi ya Rais William Ruto.

Kulingana nao, rais aliahidi watakuwa wanapewa Sh2 bilioni kila wiki.Wabunge hao kutoka vyama vyote vya kisiasa ikiongozwa na chama tawala cha UDA walisema suala hilo si la kisiasa bali kupigania haki za Wakenya.

Alisema wamepewa Sh7 milioni ambayo Sh2 milioni inatumika kwenye afisi ya wabunge huku Sh5 bilioni ikiwa hazina ya fedha ya maendeleo.

“Inasikitisha kuwa shule zimefunguliwa lakini wanafunzi wengi wamesalia nyumbani kufuatia ukosefu wa karo. Wanafunzi wengi hutegemea basari ambayo inatoka kutoka hazina hiyo. Ilikuwa tunatarajia Sh50 milioni, kususia mkutano huu si swala la kisiasa,” alisema Bw Sirma.

Bw Sirma ambaye pia ni mbunge wa Eldama Ravine alisema hawawezi kustarehe kwenye hoteli za kihafari ilhali wapiga kura wakiteseka na uchochole.

“Iwapo kufikia kesho hatutakuwa tumepokea fedha hizo tutatoka hotelini kwenda kwneye maeneo yetu ya bunge kulia na wananchi wetu. Tumekasirika sana na hatua ya Wizara ya Fedha ya kutucheleweshea fedha za kusaidia watu wetu,” aliongeza.

Mbunge wa Marakwet Kusini Bw Timothy Kipchumba alisema ni kinaya kwa serikali kutumia mabilioni ya fedha kupeleka wabunge hoteli za kifarahi ilhali yahsindwa kuwalipia wanafunzi karo za shule.

Walimlaumu Waziri wa Fedha Prof Njuguna Ndung’u kwa masaibu yao.

“Amekuwa akituahidi kuwa tutapokea fedha hizo lakini kumbe ni urongo tu. Tulichaguliwa na wakenya sababu ya kusema tutaokoa maisha ya mahasla kumbe sasa tunawakandamiza. Tumegoma hadi pale matakwa yetu yatakapotimizwa,” alisema Mbunge huyo.

Mwenzake wa Karachuonyo Bw Andrew Okuome alisema wataenedelea kususia vikao vya bunge hadi pale serikali itakapotimiza ahadi.

“Rais Ruto atomize ahadi. Hatutaki siasa hili ni swala la maisha ya watoto wetu. Tumevumilia ya kutosha, ahadi ni deni. Kwanini nilale hapa katika hoteli ya kifarahi ilhali watoto katika eneo bunge langu wanalia?” aliuliza.

Mbunge wa Wajir Kaskazini Bw Ibrahim Saney alisema sehemu kame mwa Kenya zimeathirika pakubwa na janga la ukame swala ambalo serikali inafaa kutilia maanani ili kuokoa maisha na mifugo.

  • Tags

You can share this post!

Atletico yakung’uta Real Valladolid katika La Liga na...

Wafanyakazi wa kaunti wakaa njaa kwa miezi 2 sasa

T L