• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 8:57 PM
Chama cha wafanyabiashara wa China nchini Kenya chatoa msaada kwa polisi

Chama cha wafanyabiashara wa China nchini Kenya chatoa msaada kwa polisi

 

Wawakilishi wa Chama cha wafanyabiashara wa China nchini Kenya wanaotoka mikoa ya Sichuan na Chongqing (CHUAN YU) wametoa msaada wa ofisi ya hema, meza, viti na barakoa kwa kituo cha polisi cha kilimani mjini Nairobi.

Msaada huo ni sehemu ya mchango wao wa kusaidia maafisa wa polisi kukabili janga la corona.

Wanachama wa CHUAN YU wanafuata wito wa China wa “Kijiji kimoja duniani na jamii yenye hatima moja”.

Ofisa wa makao makuu ya polisi Bwana Otieno akipongeza chama hicho alisema walipopata ugumu katika kupambana na janga la Covid-19, chama cha CHUAN YU ilijibu maombi yao kwa wakati na haraka ikaunda ofisi ya hema ya wazi, iliyo na meza na viti na kuwawezesha kuendelea na kazi yao kwenye mazingira salama.

Alisema daima watakumbuka msaada huo kama ishara ya urafiki kati ya watu wa Kenya na China.

CRI

  • Tags

You can share this post!

Afueni kwa wakazi Githurai 45 barabara zikiendelea...

Wetang’ula awasaliti UhuRaila na msimamo wa OKA