• Nairobi
  • Last Updated May 9th, 2024 6:40 PM
Chanjo mpya ya Cuba kwa jina Abdala yaibua gumzo mtandaoni

Chanjo mpya ya Cuba kwa jina Abdala yaibua gumzo mtandaoni

MDAHALO mkubwa umeibuka mtandaoni kuhusu jina la chanjo mpya ya corona kutoka Cuba ambayo imetajwa kuwa na ufanisi wa asilimia 92 katika kupambana na virusi hivyo mwilini.

Chanjo hiyo imepewa jina Abdala na inatolewa mara tatu ingawa Shirika la Afya Duniani (WHO) bado halijapendekeza matumizi yake katika kupambana na corona.Tayari chanjo hiyo imeibuka kuwa maarufu mno kutokana na jina hilo, mataifa mengi yakionyesha nia ya kuiagiza. 

Aidha waumini wa dini ya Kiislamu wamechangamkia chanjo hiyo na sasa wanataka herufi ‘h’ iongezwe ili liwe Abdalah kudhihirisha kuwa kwa kweli inamaliza virusi hivyo vinavyoendelea kusababisha vifo vingi kote ulimwenguni.

“Hatimaye badala ya Johnson and Johnson sasa tuna chanjo ya Abdala and Abdala,” akasema @adham mtandaoni.“Kwa kuwa sasa tuna chanjo ya Abdala, pia tunahitaji chanjo nyingine kwa jina Eric,” akasema @EricBana.

Kile wengi hawafahamu kwamba jina Abdala lina maana ya kihistoria kwa raia wa Cuba. Kulingana na ripoti ya chombo cha habari cha kimataifa, CNN, jina hilo linatokana na shairi la mwanawageuzi wa taifa hilo Jose Marti.

Bw Marti alikuwa mwanaharakati aliyesifiwa kwa kuchangia mageuzi nchini Cuba mnamo 1895 na alikuwa mstari wa mbele kupigania uhuru wa nchi hiyo kutoka kwa Uhispania. Alifariki wakati akishiriki vita hivyo vya ukombozi.

  • Tags

You can share this post!

Kituo cha polisi chafungwa kutokana na corona

Kingi adai serikali ilinyakua ekari 237 za wenyeji