• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 2:03 PM
Kituo cha polisi chafungwa kutokana na corona

Kituo cha polisi chafungwa kutokana na corona

Na DERICK LUVEGA

KITUO cha polisi cha Embali, eneobunge la Emuhaya, Kaunti ya Vihiga kimefungwa kwa siku 14 baada ya maafisa watatu kupatikana na virusi vya corona.

Afisa Mkuu wa Polisi wa Emuhaya, Reuben Kemboi alisema kuwa kutokana na hilo, polisi sasa watawahudumia raia katika kituo jirani cha Emaka. Polisi waliopatikana na virusi hivyo wanaendelea kujitenga nyumbani na wanaendelea vyema.

Bw Kemboi alisema maafisa wa afya wamenyunyuzia dawa ya kuua viini mazingira yote ya kituo hicho cha polisi ikiwemo seli na kitafunguliwa baada ya siku 14.“Tuliwajuza maafisa wa afya ambao walifika katika kituo cha polisi na wakainyunyuzia dawa.

Shughuli nyingi sasa zitaendelea katika kituo cha polisi cha Emaka huku tukisubiri siku 14 zikamilike ndipo ziendelee kama zamani,” akasema Bw Kemboi.Afisa huyo aliwataka raia waendelee kuzingatia masharti ya kuzuia kuenea kwa maambukizi ya corona.

Kati ya masharti hayo ni kuvaa maski, kuketi umbali wa mita moja unusu na kuosha mikono kila mara.Gavana wa Vihiga Wilber Ottichilo amekuwa akilalamikia kupanda kwa maambukizi ya corona katika kaunti hiyo, akihoji kwamba huenda kitengo cha kuwatenga wagonjwa kwenye hospitali ya Mbale, kikalemewa kuwasitiri wagonjwa wengine zaidi.

Tayari wagonjwa 13 wapo katika wodi ambako wametengwa na kuna hofu idadi hiyo ikapanda zaidi siku zinavyosonga.

 

  • Tags

You can share this post!

Sofapaka kukabili Ulinzi, Gor na AFC wakipambana na...

Chanjo mpya ya Cuba kwa jina Abdala yaibua gumzo mtandaoni