• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 7:50 AM
Dereva ashtakiwa kwa kuiba sukari ya Sh3.2 milioni

Dereva ashtakiwa kwa kuiba sukari ya Sh3.2 milioni

DEREVA ameshtakiwa kuiba sukari ya thamani ya Sh3 milioni.

Sammy Kiplagat Yego alikana kwamba aliiba sukari ya kampuni Maisha Steel East Africa Limited.

Yego alikabiliwa na shtaka mnamo Mei 25, 2022 aliiba bandali 620 za sukari.

Sukari hiyo ilikuwa imetengenezwa na kiwanda cha Kabras.

Hakimu mkazi Mahakama ya Milimani Carolyne Muthoni Njagi alifahamishwa mshtakiwa aliiba sukari hiyo ya thamani ya Sh3,224,000.

Upande wa mashtaka umeelezwa sukari hiyo ilikuwa inasarishwa kutoka kiwanda cha West Kenya Limited ilipomea miguu.

Sukari hiyo ilitoweka kwenye barabara ya Kakamega-Nairobi.

Yego anadaiwa alishirikiana na watu wengine ambao hawakufikishwa kortini wakati wa kutekeleza wizi huo.

Sukari hiyo ilikuwa inasafirishwa kutoka kiwanda cha West Kenya Sugar Company Limited ikipelekwa kampuni ya Siana Trading Company, Nairobi.

Yego alikanusha shtaka dhidi yake.

Aliomba aachiliwe kwa dhamana.

Bi Njagi alimwachilia kwa dhamana ya Sh1 milioni na mdhamini mmoja wa kiasi sawa na hicho ama alipe dhamana ya pesa taslimu Sh800,000 ili aachiliwe kutoka korokoroni.

Kesi itatajwa katika muda wa wiki mbili kutengewa siku ya kusikilizwa.

  • Tags

You can share this post!

Sekta ya kilimo imepuuzwa – Ruto

Kihara aomba kesi ya Sonko izamishwe

T L